MASOMO YA MISA, OKTOBA 6, 2021
JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA
Yon. 4:1-11
Yona alikasirika sana. Akamwomba Bwana,
akasema, Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika
nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana
nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira,
u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba,
uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Naye Bwana akasema, Je! Unatenda vema
kukasirika? Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji,
akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule
utakuwaje. Na Bwana Mungu aliweka tayari mtango, akaufanya ukue juu ya Yona,
ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumponya katika hali yake mbaya. Basi
Yona akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango. Lakini siku ya pili
kulipopambazuka, Mungu akaweka tayari buu, nalo likautafuna ule mtango,
ukakauka.
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu
akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona
kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa akajitakia kufa, akasema, Ni
afadhali nife mimi kuliko kuishi. Mungu akamwmbaia Yona, Je! Unatenda vema
kukasirika kwa ajili yam tango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika
hata kufa.
Bwana akamwmbia, Wewe umeuhurumia
mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuutesha; uliomea katika usiku mmoja, na
kuangamia katika usiku mmoja; na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji
ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza
kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tenda wamo
wanyama wa kufugwa wengi sana?
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 86:3-6, 9-10 (K) 15
(K) Wewe Bwana, u Mungu wa rehema na
neema.
Wewe, Bwana, unifadhili,
Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.
Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,
Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe,
Bwana. (K)
Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,
Umekuwa tayari kusamehe.
Na mwingi wa fadhili,
Kwa watu wote wakuitao.
Ee Bwana, uyasikie maombi yangu;
Uisikilize sauti ya dua zangu. (K)
Mataifa yote uliwafanya watakuja;
Watakusujudia Wewe, Bwana.
Watalitukuza jina lako;
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu.
Wewe ndiwe mfanya miujiza,
Ndiwe Mungu peke yako. (K)
SHANGILIO
Ebr. 4:12
Aleluya, aleluya,
Neno la Mungu li hai tena li na nguvu,
li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.
INJILI
Lk. 11:1 – 4
Yesu alipokuwa mahali fulani akiomba,
alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi
kusali, kama vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, Msalipo,
semeni: Baba, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Utupe siku kwa siku riziki
yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na
usitutie majaribuni.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment