“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Ijumaa, Octoba 29, 2021,
Juma la 30 la Mwaka
Roma: 9: 1-5;
Lk 14: 1-6.
KUWA NA HURUMA
Leo Yesu anwauliza Mafarisayo swali “je,
ni kinyume cha sheria kumponya mtu siku ya Sabato?” Mafarisayo hawana jibu.
Baada ya kumponya mtu aliyekuwa na ukoma, anawaonya Mafarisayo kwa kushindwa
kuonesha huruma, na badala yake kutumia sababu za kisheria.
Mafarisayo hawakuwa na huruma kwa ndugu
zao, huyu mtu mwenye ukoma, walikuwa wakijishughulisha na Sabato. Yesu
anawauliza kwa mfano alikuwa mwana wao au alikuwa ni punda wao? Yesu anaonesha
mioyo baridi ya Mafarisayo, ambao walifikiria kwamba punda ni zaidi ya wana wa
Mungu waliokuwa wagonjwa na maskini.
Kama tukijaribu kumwangalia huyu mtu
alieponywa. Ugonjwa ambao ulikuwa ukimtesa ulikuwa ni ukoma, ambapo mwili hutoa
maji maji. Sisi kama Mafarisayo huenda tukawa tunaugua ugonjwa kama wa
Mafarisayo-pengine si katika hali ya mwili. Hili linakuja pale ambao tunajaza
mioyo yetu na ubinafsi na kushindwa kupenda kizuri kwa ajili ya wengine. Ni
Yesu mwenyewe anayeweza kuondoa ukame wetu na ubinafsi wetu wa kushindwa
kuwapenda wengine kwa uhuru.
Cha muhimu ni kuona mwitikio wetu juu ya
wale wanao hitaji msaada wetu, huwa tuna visingizio vingi vya kutoa. Kwa mfano
swala la wakimbizi, Baba mtakatifu Fransisko la kuwasahauri parokia na wakristo
kuwakaribisha wakimbizi halikupokelewa sana. Swala hili wamelichukulia katika
mijadala. Lakini mbaya zaidi hakuna hata tendo lolote la huruma wanalopendekeza
wale wanao pinga.
Leo, tujiulize sisi wenyewe kama nasi
tuna mioyo baridi. Je, tupo tayari kuvuka mipaka ya akili zetu na mipaka ya
roho zetu kwa aili ya kuwa wakarimu?
Sala: Bwana Yesu njoo katika moyo wangu,
katika hali yangu ya maisha. Njoo zama, katika kazi, kati ya marafiki, katika
magumu yangu, wakati wa matatizo, na katika vitu vyangu. Nisaidie mimi niweze
kuwa mkarimu kwa ndugu zangu. Yesu, nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment