“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Ijumaa,
Oktoba 22, 2021
Juma
la 29 la Mwaka
Rom
7: 18-25;
Zab
119: 66, 76-77, 93-94 (K) 68;
Lk
12: 54-59.
KUFAFANUA
NYAKATI ZETU
Leo
katika Injili ya Luka inafafanua ni kwa jinsi gani baadhi ya watu walikuwa na
uwezo wakusoma majira kwa mfano mawingu na mvua kipindi cha Yesu, lakini wakashindwa kufafanua kipindi cha Yesu ambacho
Yesu mwenyewe alikiweka mbele ya macho yao kwa kuhubiri Neno la Ufalme wa
Mungu. Je, si kweli kwa nyakati zetu
pia?
Sisi
tumebobea sana katika teknologia ya sayanzi na tunajivunia sana hali hii.
Lakini mara nyingi tunakosa ujumbe ambao Mungu anataka kutuambia. “alama za nyakati” ulikuwa ni ujumbe muhimu
sana wakati wa mkutano wa Vatican II ukituita kufafanua Neno la Mungu kulingana
na nyakati zetu bila kuharibu ujumbe wa
Yesu na mtazamo wa kanisa la kwanza na ujumbe wa Mababa wa kanisa. Kufafanua wakati
wetu maana yake kujikabidhi wenyewe kwenye ukweli. Tunapaswa kumtafuta Yesu kwa
moyo wote na kutaka yale yote ambayo yapo kwa ajili yake na kuacha yale yasio
ya kwakweli.
Jamii
yetu inatuwekea maadili mbali mbali, tunaweza kujikuta sisi tukivutwa huku na
huku. Tunaweza kukuta kwamba akili zetu zimechukuliwa na tukakuta hata kile
muhimu cha ubinadamu wetu kimeharibiwa. Mfano sheria za kutoa mimba, kuwaua
watu kwa sindano eti kisa anateseka mno! Ndoa za kijadi! Maadili yetu yamevamiwa katika kila nyanja.
Kusoma alama za nyakati ni kuwa makini na kuyaona yote jinsi ulimwengu unavyo
jichanganya kila wakati na kulinda ukweli. Huku tukiona makosa yanayoletwa
kwenye maadili na tamaduni zetu.
Tafakari
leo kama upo tayari kumkaribisha Roho wa ukweli akuongoze katika kweli.
Kuutafuta ukweli na kubaki nao ndio njia pekee ya kulinda maadili yetu na
kukwepa madhara yanaoletwa na teknolojia.
Sala:Bwana,
nisaidie niweze kusoma alama za nyakati na kuona makosa yote yanayo tokana nayo
na pia uzuri wako unaoneakana katika hilo. nipe ujasiri na nguvu niweze kukwepa
kile kilicho kiovu na kutafuta kile
ambacho kinatoka kwako. Yesu nakuamini wewe. Amina.
Copyright ©2013-2021 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment