MASOMO
YA MISA, OKTOBA 1, 2021
IJUMAA,
JUMA LA 26 LA MWAKA
SOMO
1
Bar.
1:15-22
Kwa
Bwana Mungu wetu, haki; lakini kwetu sisi haya ya uso kama hivi leo, kwa watu
wa Yuda na kwa wenyeji wa Yerusalemu, na kw awafalme wetu, na kwa wakuu wetu,
na kwa makuhani wetu, na kwa manabii wetu, na kwa baba zetu, kwa sababu
tumetenda dhambi mbele ya Bwana. Tumemwasi, wala hatukuitii sauti ya Bwana
Mungu wetu, kwenda katika sheria zake alizoziweka mbele yetu. Tangu siku Bwana
aliyowatoa baba zetu katika nchi ya Misri hata leo tumemwasi Bwana Mungu wetu
na kutenda yasiyofaa kwa kutoisikiliza sauti yake.
Kwa
hiyo mapigo haya yameshikamana nasi, na ile laana ambayo Bwana alimwamuru
mtumishi wake Musa, katika siku aliyowaleta baba zetu kutoka katika nchi ya
Misri ili atupe nchi ijaayo maziwa na asali, kama hivi leo. Lakini
hatukuisikiliza sauti ya Bwana Mungu wetu, kwa kuyafuata maneno yote ya manabii
aliyotupelekea, bali tulikwenda kila mtu katika mawazo ya moyo wake mbaya,
kutumikia miungu ya kigeni na kufanya yaliyo maovu machoni pa Bwana Mungu wetu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
79:1-6, 8-9 (K) 9
(K)
Utusaidie, Ee Mungu, kwa ajili ya utukufu wa jina lako.
Ee
Mungu, mataifa wameingia katika urithi wako,
Wamelinajisi
hekalu lako takatifu.
Wamefanya
Yerusalemu chungu chungu.
Wameziacha
maiti za watumishi wako
Ziwe
chakula cha ndege wa angani.
Na
miili ya watauwa wako Iwe chakula cha wanyama wa nchi. (K)
Wamemwaga
damu yao kama maji
Pande
zote za Yerusalemu,
Wala
hapakuwa na mzishi.
Tumekuwa
lawama kwa jirani zetu,
Mzaha
na dhihaka kwao wanaotuzunguka.
Ee
Bwana, hata lini? Utaona hasira milele?
Wivu
wako utawaka kama moto? (K)
Usikumbuke
juu yetu maovu ya baba zetu,
Rehema
zako zije kutulaki hima.
Kwa
maana tumedhilika sana. (K)
Ee
Mungu wa wokovu wetu, utusaidie,
Kwa
ajili ya utukufu wa jina lako.
Utuokoe,
utughofiri dhambi zetu,
Kwa
ajili ya jina lako. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya,
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Lk.
10:13 – 16
Yesu
aliwaambia wafuasi wake: Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama
miujiza hiyo iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni,
wangalitubu tangu hapo, huku wakiketi katika nguo za kigunia na majivu. Lakini,
siku ya hukumu itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zake kuliko
ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa hata mbinguni? Utashushwa hata kuzimu.
Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye
anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment