“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Ijumaa,
Septemba 24, 2021
Juma
la 25 la Mwaka
Lk
9: 18-22
KRISTO
NI NANI KWANGU?
Karibuni
sana ndugu wapendwa kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la
Bwana leo katika somo la kwanza Nabii anawatia moyo viongozi wa taifa la Yuda
kwamba wasiogope ati watapata mali wapi ili waweze kulijenga hekalu la Bwana.
Bwana ataagiza mali, na utukufu wote toka katika mataifa kuja kulijia hekalu la
Yerusalemu na kulifanya lingae na kupambika kwani dhahabu ni ya Bwana, na kila
utajiri uliopo kati ya mataifa ni mali ya Bwana pia. Hivyo Bwana aweza
kuuchukua na kuuleta Yerusalem upambe hekalu lake.
Somo
hili litufanye tuwe watu wenye kufanya bidiii zaidi tutambue kwamba tunapaswa
kujitoa kwa ajili ya Bwana zaidi na zaidi ili kulifanya hekalu la Bwana
lipendeze vyema. Hatupaswi kuogopa au kuona ugumu katika kumpatia Bwana
kilichochake, Bwana apewe dhahabu na fedha yake, wapo wengi wamejidai kumnyima
Bwana dhahabu na fedha yake bila kumtolea chochote lakini mwisho wa siku,
wameviacha vitu hivi hapa ulimwenguni kwani vinabakia kuwa mali ya Bwana. Hivyo
tukiwa hapa duniani, tukumbuke kuwa ni Mungu ameamua kutukabidhi ili tuvitunze.
Tuache kujisahau na kufikiria kwamba ni vyetu. Hapana, tutaviacha hapa hapa.
Fedha
na mali yote ni vya Bwana. Hivyo tusiache kumpa Bwana kilicho chake. Hata muda
na vipaji tulivyonavyo ni kwamba tumekabidhiwa ili tumtunzie Bwana na ipo siku
atavichukua. Na hivyo tusiishi kana kwamba ni vyetu na kwamba hatutakaa
vichukuliwe toka kwetu. Hivyo tusisahau kutoa kwa ajili ya maskini kwa kila
siku.
Katika
somo la injili, Petro anamkiri Yesu waziwazi kwamba yeye ni masiha. Sisi
tunapaswa kuwa kama Petro, yafaa tumkiri Yesu kuwa Kristo kwetu. Yesu kwa kila
wakati anaigwa na wengi na hivyo waamini wanaoweweseka watashindwa kumtambua
Yesu ni yupi. Wapo wanaofikiri kwamba yeye ni Yohane mbatizaji, wengine Elia na
wengine ni mojawapo wa manabii. Na hawa watajitokeza hivihivi pia wakidai
kwamba wao ni Yesu. Sisi tunapaswa kuwa makini, tukitambua kwamba Bwana Yesu
kwa wakati wote wapo wanaotamani kumwiga, kuiga jina lake na ukuu wake. hivyo
tumkiri Kristo kweli. Tuachane na matapeli.
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment