Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

Je, wewe ni Jiwe la kuzuia wengine au Jiwe la kuvushia wengine?

 *MBEGU ZA UZIMA*. TAFAKARI YA DOMINIKA YA 26 YA MWAKA WA KANISA


Je, wewe ni Jiwe la kuzuia wengine au Jiwe la kuvushia wengine? 


Ulimwengu umekuwa mdogo sana. Watu wanaishi karibu zaidi kuliko zamani. Wanahitajiana kila siku hata zaidi ya zamani. Kwa hiyo kila mmoja anahitajika kwa hali kubwa. Mkristo anapaswa kutambua kwamba namna anavyoishi inagusa maisha ya mwingine labda kwa uzuri kama anaishi vizuri au kwa ubaya kama anaishi vibaya. Nipende nisipende naweza kuwa jiwe la kuzuia kwa ndugu zangu au jiwe la kuwavusha wengine katika barabara ya wokovu. Hili ni muhimu kwa watu wa aina zote: wadogo, wakubwa, wenye ndoa, wazazi, walioajiriwa, n.k. 

Mmoja anaweza kuwa jiwe la kuzuia namna gani?


1. Wakati tunapokuwa sio wakarimu na wasio haki. Tunawakwaza wadogo na kuharibu utu wao na kuharibu ujasiri wao. 


2. Tunaposhindwa kuelewa mapungufu ya wengine, maanguko yao, dhambi zao na kuwatupilia mbali. Tunapowahukumu wengine na kujifanya wajione wao kuwa waovu kupita kiasi. 


3. Tunapowahukumu wengine kwa sababu hawaishi kama tunavyopenda. Tunawaumiza na kuharibu taswira yao. 


4. Tunapowakatisha tamaa wengine, kuwaweka chini na kuwafanya wasiinuke. Pale tunapozuia mwanga wao na kujikuta wakitembea katika giza na kujihisi wanyonge. 


5. Wakati unapowakataa wengine, tunapowatenga na kuwakataa. Tunawafanya wajisikie kama waliokataliwa na wasiofaa. 


6. Wakati tunapowakosoa wengine kwa upinzani mkali bila kuwa na mapendo. Tunararua kabisa mawazo yao na sisi kuwa kovu katika matumaini yao. 


7. Tunapowanyonya wengine kwa kuwalipa mshahara kidogo. Tunawafanya wawe kama watumwa na sisi kuishi kama mabwana. Tunawakandamiza ili sisi tubaki na nguvu. 

Tukifanya kati ya haya kwa wengine, sisi tunakuwa giza kwao na kuzuizi katika njia zao. Tunawafanya waone ugumu katika kuufikia Ufalme wa Mbinguni. 


Lakini, pia tunaweza kuwa jiwe la kuvushia wengine. 


1. Tunapowasaidia wengine wakati wa madhaifu na wasiwasi. 


2. Tunapoinua ujasiri wao na kuwafanya watambue vipaji vyao. 


3. Tunapowapa changamoto na kuwasaidia kukua katika mawazo sahihi. 


4. Tunapokataa kujiunga na makundi ya kuwarushia mawe au lawama kwa sababu ya dhambi zao. 


5. Tunapowasamehe. Tunawanasua kutoka katika mambo yao ya zamani na kuwafanya wasonge mbele. 


6. Wakati tunapo waelewa na kuwasikiliza na wao kujisikia kama sisi ni dada na kaka kwao. 


7. Wakati tunapo kataa kuwanyanyasa au kujichukulia umaarufu kwa sababu ya mapungufu yao. 

Kama tumefanya kati ya haya kwao, sisi tumekuwa mwanga kwao. Sisi tunakuwa kama kibao cha kuelekeza wakati wakiwa katika matatizo na mashaka. Tunakuwa kama kivuko kwao katika mawimbi mengi ya dhoruba za maisha. Sisi tunakuwa mfano kwao na rafiki wa kweli.


Yesu anasema kwamba kama mmoja akimpatia kikombe kidogo cha maji ya baridi atarudishiwa daima. Tunapaswa kufanya hivyo kwa kuwaelekeza wengine katika kisima chetu na kuwashirikisha maji. Tafakari leo juu ya mahusiano yako. Kama una rafiki wa karibu katika maisha yako, tafakari jinsi unavyomsaidia. Hakikisha Yesu yupo katika mahusiano yenu. 


Sala: Baba wa Mbinguni, sisi ni wadhaifu daima tuliotiwa sumu na dhambi. Tunaomba neema ili tusiweze kuangushwa chini wala kuwaangusha wenzetu kwenye dhambi, Amina.

No comments:

Post a Comment