MASOMO YA MISA,
IJUMAA, AGOSTI 20, 2021
JUMA LA 20 LA MWAKA
________
SOMO I
Rut 1: 1, 3-6, 14-16, 22
Ikawa zamani za Waamuzi
walipoamua, kulikuwa na njaa katika nchi. Akaondoka mtu mmoja wa Bethlehemu ya
Yuda, akaenda kukaa katika nehi ya Moabu, yeye na mkewe na wanawe wawili. Akafa
Elimeleki, mumewe Naomi; na yule mwanamke akasalia na wanawe wawili. Nao wakaoa
wake katika wanawake wa Moabu; na jina la mmoja aliitwa Orpa, na jina la wa
pili Ruthu. Wakakaa huko yapata miaka kumi. Wakafa na Maloni na Kilioni wote
wawili; na huyo mwanamke akawa amefiwa na wanawe wawili, na mumewe pia.Ndipo
alipoondoka, yeye na wakueze, ili kurudi kutoka nchi ya Moabu; maana huko katika
nchi ya Moabu amesikia ya kwamba Bwana amewajilia watu wake na kuwapa chakula.
Orpa akambusu mkwewe. akarejea kwa watu wake, lakini Ruthu akaambatana naye.
Naye akasema. Tazama.
shemeji yako amerejea kwa watu wake, na kwa mungu wake; basi urejee wewe
umfuate shemeji yake. Naye Ruthu akasema. Isinisihi nikuache, nirejee
nisifuatane nawe; maana wewe uendako nitakwenda. na wewe ukaapo nitakaa. Watu
wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.
Basi Naomi..akarudi;
pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao
wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri.
Neno la
Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO WA KATIKATI
Zab 146 : 5-10(K) 2
(K) Ee nafsi yangu,
umsifu Bwana.
Heri ambaye Mungu wa
Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa
Bwana, Mungu wake.
Aliyezifanya mbingu na
nchi,
Bahari na vitu vyote
vilivyomo. (K)
Huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu
waliooncwa,
Huwapa wenye njaa
chakula;
Bwana hufungua
waliofungwa. (K)
Bwana huwafumbua macho
waliopofuka;
Bwana huwainua
walioinama;
Bw ana huwapenda wenye
haki;
Bwana huwahifadhi wageni;
Huwategemeza yatima ya
mjane. (K)
Bali njia ya wasio haki
huipotosha.
Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, Ec Sayuni.
kizazi hata kizazi.
Aleluva. (K)
________
SHANGILIO
Zab 27:11
Aleluya, aleluya,
Ee Bwana, unifundishe
njia yako,
na kuniongoza katika njia
iliyonyoka.
Aleluya.
________
INJILI
Mt. 22: 34-40
Mafarisayo waliposikia ya
kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. Mmoja wao,
mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo
kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na
yapili yafanana nayo, ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri
hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Copyright © 2020,
"MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment