Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Agosti 8 2026
Juma la 18 la Mwaka
Zab. 9 : 7-12 (K) 10;
Mt 17: 14-20.
Katika Injili ya leo,
baada ya wanafunzi wa Yesu kurudi katika utume wao, walishangaa kwanini
hawakuweza kumponya kijana aliyekuwa ana pepo mchafu. “kasababu ya Imani yenu
ndogo” Yesu aliwaambia. Mngekua na Imani ndogo kama chembe ya haradani”
aliwaambia, “hakuna chochote ambacho kingeshindikana kwenu”.Mwaliko huu wa Yesu
sio kiingiilio cha kumpa rushwa Mungu atafanyie maajabu, bali ni mwito wa
kuweka matumaini yetu yote kwake kwa chochote kitokeacho kwetu, yeye tayari
ajua lipi bora kwetu kulingana na mapenzi yake.Imani hii ikiwa ndani ya upendo
mkuu, ndio iletayo furaha na amani katika maisha yetu, hata katika kipindi
kigumu cha maisha yake.
Sala: Ee Bwana,
Nakutumainia wewe. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2026
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment