“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumamosi, Julai 3, 2017,
Juma la 13 la Mwaka
Sikukuu ya Mt. Toma,
Mtume
Efe 2:19-22
Zab 117:1-2;
Yn 20:24-29.
KUTOA USHUHUDA KWA YESU
MFUFUKA!
Leo tuna sheherekea
sikukuu ya Mt. Thomasi, Mtume. Thomas ni maarufu sana kwa maswali yake
aliyeyaleta, na tunaweza kutulia kwasababu ya maneno ya kwanza aliyosema Yesu,
wakti Tomasi akiwa na mashaka: “Amani iwe nanyi”. Yesu hakumwaibisha au kupatwa
na hasira bali alimpa Amani. Yesu ambaye anatufahamu sisi katika ubinadamu wetu
na ambaye anatufahamu undani wetu kabisa, anatupatia sisi amani wakati tukiwa
katika hofu na mashaka yetu. Wakati Thomasi anatoa ishara kwa ajili ya ombi
lake la kuingia katika hali hiyo ya Imani au kuamini, haombi kitu kigeni zaidi
ya ile Imani ambayo kila mfuasi alikuwa ameshapokea. Ni wazi kwamba yeye
alitaka kupata naye muda wakushuhudia kama wengine walivyo fanya-kabla haja
amini jambo hilo kubwa linalo shangaza.
Lakini tukio haliishi
hapa, kwa Yohane au kwa Bwana mfufuka mwenyewe anaendelea na kusema “je, una
amini kwasababu umeniona? Wana heri wale wasio ona na kuamini”. Kwetu sisi
maneno haya ni ya muhimu sana. Kwasababu hatukuona, sasa inakuwaje tuna amini?
Tomasi hakuweza kuamini mpaka alipo ona. Petro hakuweza kaumini mpaka alivyo
ona. Maria Magdalena hakuweza kuamini mpaka alivyo ona. Sasa tuta aminije
wakati sisi hatujaona? Inawezekana kwasababu sisi tumesha barikiwa,
“wamebarikiwa wale wasio ona lakini wana amini.”. Ni lazima tutambue na
kukubali kwamba Imani yetu sio kutokana na juhudi zetu wenyewe au labda dini
tunayo fuata bali ni “zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu”. Mungu Baba ametupa
kitu ambacho kina saidia Imani yetu kwa Bwana mfufuka iwezekane-hata pale
ambapo hatuja muona Yesu mfufuka kwa macho yetu ya kibinadamu.
Sala: Bwana, imarisha Imani
yangu kama Tomasi alivyolia “Bwana wangu na Mungu wangu”. Yesu nakuamini wewe.
Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment