MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2025
JUMATATU,
JUMA LA 13 LA MWAKA
SOMO
1
Mwa.
18:16-33
Watu
hao waliondoka huko wakaelekeza nyuso zao Sodoma. Ibrahimu akaenda pamoja nao
awasindikize. Bwana akanena, Je! Nimfiche Ibrahimu jambo nilifanyalo, akiwa Ibrahimu
atakuwa taifa kuu, hodari, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?
Kwa maana nimemjua ya kwamba atawaamuru wanawe, na nyumba yake baada yake
waishike njia ya Bwana, wafanye haki na hukumu, ili kwamba Bwana naye
akamtimizie Ibrahimu ahadi zake. Bwana akasema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na
Gomora kimezidi, na dhambi zao zimeongezeka sana, basi, nitashuka sasa nione
kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua.
Basi
wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali
akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye
haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu,
wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Hasaha, usifanye
hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha;
Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma
wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
Ibrahimu
akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu
tu. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, je! Utaharibu mji
wote kwa kpungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano.
Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema,
Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami
nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo
thelathini. Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko
ishirini? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Akasema, Bwana asiwe
na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema,
Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.
Basi
Bwana alipokwisha kuzungumza na Ibraimu, akaenda zake; Ibrahimu naye akarudi
mahali pake.
Neno
la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
103:1-4, 8-11 (K) 8
(K)
Bwana amejaa huruma na neema.
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Naam,
vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi
jina lake takatifu.
Ee
nafsi yangu, umhimidi Bwana,
Wala
usizisahau fadhili zake zote. (K)
Akusamehe
maovu yako yote,
Akuponya
magonjwa yako yote,
Aukomboa
uhai wako na kaburi,
Akutia
taji ya fadhili na rehama. (K)
Bwana
amejaa huruma na neema,
Haoni
hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.\yeye hatateta sikuzote,
Wala
hatashika hasira yake milele. (K)
Hakututenda
sawasawa na hatia zetu,
Wala
hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.
Maana
mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,
Kadiri
ileile rehema zake ni kuu kwa wamchao. (K)
SHANGILIO
Yn.
10:27
Aleluya,
aleluya.
Kondoo
wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.
Aleluya.
INJILI
Mt.
8:18 – 22
Yesu
alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng’ambo. Mwandishi
mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata kokote uendako. Yesu
akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana vioto; lakini Mwana wa
Adamu hana pa kulaza kichwa chake.
Mwingine
katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike
baba yangu. Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.
Neno
la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright
© 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment