Everyday Saint / Maisha ya Watakatifu

MASOMO YA MISA, JUNE 27, 2021.

 MASOMO YA MISA, JUNE 27, 2021.


DOMINIKA YA 13 YA MWAKA B WA KANISA


MWANZO:

Zab. 47:2

Enyi watu wote pigeni makofi, mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe.


SOMO 1

Hek. 1:13-15; 2 : 23-24


Mungu hakuifanviza mauti, wala haimpendezi walio hai wakipotea. Kwa maana aliviumba vitu vyote ili vipate kuwako, na nguvu za uzazi zilizomo ulimwenguni ni za kuleta siha, wala hakuna ndani yake sumu yo yote ya uharibifu. wala ahera haina milki kama ya kifalme hapa duniani; Maana haki yaishi milele. Yaani, Mungu alimwumba mwanadamu ili apate kutokuharibika, kwa mfano wake mwenyewe, ila ulimwengu uliingiwa na mauti kwa husuda kuionja.


Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.


WIMBO WA KATIKAT1 

Zab. 30: 1, 3-5, 10-12 (K) 1


(K) Ee Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua.


Bwana, nitakutukuza kwa maana umeniinua,

Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.

Umeniinua nafsi yangu,

Ee Bwana, kutoka kuzimu.

Umenihuisha na kunitoa

Miongoni mwao washukao shimoni. (K)


Mwimbieni Bwana zaburi,

Enyi watauwa wake.

Na kufanya shukrani.

Kwa kumbukumbu la utakatifu wake.

Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo,

Katika radhi yake mna uhai.

Huenda kuliko huja kukaa usiku,

Lakini asubuhi huwa furaha. (K)


Ee Bwana, usikie, unirehemu,

Bwana, uwe msaidizi wangu.

Uligeuza matanga yangu kuwa machezo;

Ee Bwana, Mungu wangu,

Nitakushukuru milele. (K)


SOMO 2 

2 Kor. 8 : 7, 9,13-15


Kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia. Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. Maana sisemi bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa. Kama ilivyoandikwa, aliyekusanya vingi, hakuzidi, wala yeye aliyekusanya vichache hakupungukiwa.


Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.


SHANGILIO 

Yn. 1 :12,14


Aleluya, aleluya, 

Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu. Wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu. 

Aleluya.


INJILI 

Mk. 5 :21-4:


Yesu alipokwisha kuvuka kurudi ng’ambo katika kile chombo, wakamkusanyikia mkutano mkuu; naye alikuwa kando ya bahari. Akaja mtu mmoja katika wakuu wa sinagogi, jina lake Yairo; hata alipomwona, akaanguka miguuni pake, akimsihi sana, akisema, Binti yangu mdogo yu katika kufa; nakuomba uje, uweke mkono wako juu yake, apate kupona, na kuishi. Akaenda pamoja naye. Mkutano mkuu wakamfuata, wakimsonga-songa. Na mwanamke mmoja mwenye kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, na kuteswa mengi kwa mikono ya matabibu wengi, amegharimiwa vitu vyote alivyo navyo, kusimfae hata kidogo, bali hali yake ilizidi kuwa mbaya; aliposikia habari za Yesu, alipita katika mkutano kwa nyuma, akaligusa vazi lake, maana aiisema, Nikiyagusa mavazi yake tu, nitapona. Mara chemchemi ya damu yake ikakauka, naye akafahamu mwilini mwake kwamba amepona msiba ule. Mara Yesu, hali akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya mkutano, akasema, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu? Wanafunzi wake wakamwambia, Je! wawaona makutano  wanavyokusonga-songa, nawe wasema, Ni nani aliyegusa? Akatazama pande zote ili amwone yule aliyelitenda neno hilo. Na yule mwanamke akaingiwa na hofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote. Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena. Halipokuwa katika kunena, wakaja watu kutoka kwa yuakole mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kusumbua mwalimu? Lakini Yesu, alipolisikia lile neno likinenwa, akamwambia mkuu wa sinagogi, Usiogope, amini tu. Wala hakumruhusu mtu afuatane naye, ila Petro, na Yakobo, na Yohane nduguye Yakobo. Wakafika nyumbani kwa yule mkuu wa sinagogi, akaona ghasia, na watu wakilia, wakifanya maombolezo makuu. Alipokwisha kuingia, akawaambia, Mbona mnafanya ghasia na kulia? Kijana hakufa, bali amelala tu. Wakamcheka sana. Naye alipokwisha kuwatoa nje wote, akamtwaa babaye yule kijana na mamave, na wale walio pamoja naye, akaingia ndani alimokuwamo yule kijana. Akamshika mkono kijana, akamwambia, Tallitha, kumi; tafsiri yake, Msichana, nakuambia, Inuka. Mara akasimama yule kijana, akaenda; maana alikuwa amepata umri wa miaka kumi na miwili. Mara wakashangaa mshangao mkuu. Akawaonya sana, mtu asijue habari ile; akaamuru apewe chakula.


Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristu.

No comments:

Post a Comment