“Mbegu
za Uzima”
Jumapili,
Mei 30, 2021
Sherehe
ya Utatu Mtakatifu
Kumb
4: 32-34,39-40;
Zab
33: 4-6,9,18-20,22(K. 13);
Rum
8:14-17;
Mt
28: 16-20.
MUNGU
UTATU MTAKATIFU!
Wakatoliki
, duniani kote, sio kwamba wanaamini Mungu tu, bali wanaamini Mungu mmoja.
Lakini Mungu wetu yupo katika Utatu- Utatu katika umoja na umoja katika Utatu.
Kila mmoja ni Mungu kwa asili na wote ni Mungu mmoja. Sawa katika Nguvu, ni wa
milele na wana utukufu. Fumbo hili kuu linaweza kuchukuliwa kama fumbo lililo
kuu kabisa katika Biblia Takatifu. Wakristo tunaamini fumbo hili kuu ndani ya
mamlaka ya Yesu Kristo na Agano Jipya. Ni moja wapo ya fumbo kubwa la ndani
kabisa lililofunuliwa na lililopo juu kabisa kupita akili ya mwanadamu. Yesu
mara nyingi ameongea kuhusu Mungu kama Baba yake. Sauti ya Baba ilisikika
wakati wa ubatizo wa Yesu; “Huyu ni mwanangu mpendwa niliye pendezwa naye
msikilizeni yeye”. Yesu alipo ngara sura, pia, sauti hiyo hiyo ilisikika
ikisema maneno hayo hayo. Katika matukio yote uwepo wa wingu jeupe ilionyesha
uwepo wa Roho Mtakatifu, ambaye Yesu aliwaahidia wakati alipokuwa akipaa kwenda
kwa Baba, “nitawapa msaidizi Mwingine-Roho wa kweli anayetoka kwa Baba”.
Yesu
anatuambia kwamba, Mungu aliupenda sana ulimwengu mpaka akamtuma mwanaye
ulimwenguni, ili wote watakao muamini wasipotee bali wawe na uzima wa milele
(Yn 3:16). Anaelezea uhusiano wake ndani ya Mungu mmoja wa kweli na anawataka
mitume na wafuasi watambue na wakubali kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwamba
Mungu ni Baba yake, na kwamba Roho Mtakatifu alitumwa kwao na Baba na Mwana.
Wakristo wa kwanza walisadiki ndani ya Utatu Mtakatifu bila kupinga. Baada ya
kuamini, kinachofuata ni Upendo. “Kama mtu akinipenda mimi” Yesu anasema, “Baba
yangu atampenda. Nasi tutakuja kwake nakufanya makao ndani yake.”
“…(Wana
ndoa) matunda ya wana ndoa yanakuwa ishara ya kuelewa na kuelezea fumbo la Mungu
mwenyewe, kwasababu kwa mtazamo wa Kikristo wa Utatu mtakatifu, Mungu
anatafakariwa kama Baba, na Mwana na Roho Upendo. Utatu Mtakatifu ni umoja wa
upendo, na familia ndiyo inayoishi kuonesha umoja huu. Mtakatifu Papa Yohane
Paulo wa Pili, alitoa mwanga kwa hili alivyosema ‘Mungu wetu katika undani wake
sio upweke bali ni familia, kwani ndani yake ana Ubaba, mwana na undani wa
familia ambaye ni Upendo. upendo huo ndani ya familia ya Kimungu ni Roho
Mtakatifu’”. (Baba Mtakatifu Fransisko katika Furaha ya upendo, Amoris
Laetitia, 11)
Tutafakari
leo juu ya sherehe hii ya Utatu Mtakatifu, ni mara ngapi nina enzi upendo huu
wa Utatu Mtakatifu katika mahusiano yangu? Tujaribu kufanya jitihada tusonge
mbele zaidi, katika mapendo yetu, na kumruhusu Mungu akupe matokeo mazuri ya
tokanayo na upendo wako kwake na kwa jirani.
Sala:
Baba na Mwana na Roho Mtakatifu, nisaidie mimi niweze kuku fahamu wewe na
kukupenda. Nisaidie niweze kuelewa upendo unaoshiriki na Mwanao. Kwa kuelewa
upendo huo, nisaidie na mimi niweze kushirikisha upendo huo kwa wengine. Baba
na Mwana na Roho Mtakatifu, nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment