“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari ya kila siku
Jumanne, Juni 4, 2024,
Juma la 9 la Mwaka
2 Pet 3: 12-15,17-18
Zab 90:2-4,10,14,16; ;
Mk 12: 13-17.
KUTEMBEA KATIKATI YA
MITEGO!
Mafarisayo na Maherodi
walijaribu kumtega Yesu katika maongezi yake. Walijaribu kutumia akili yao ili
kumfanya Yesu aongee maneno ya kumpinga Kaisari na hivyo kupata kisingizio cha
ugomvi na utawala wa Kirumi. Lakini chakushangaza walichokuwa wakisema kuhusu
Yesu kilikuwa cha kweli na ilikuwa fadhila kubwa.
Walisema mambo mawili
ambayo yalionesha unyenyekevu wa Yesu na uaminifu wake: “twajua ya kuwa wewe u
mtu wa kweli,” na “wala hujali cheo cha mtu; kwa maana hutazami sura za watu;
lakini katika kweli waifundisha njia ya Mungu”. Yesu haingii katika mtego wao
na anafanya kwa hekima kubwa na kumalizana nao.
Tukitafakari juu ya
fadhila hizi mbili, tunatambua kuwa maisha yetu ni mara chache sana yanakuwa
namna hiyo. Kwanza kabisa, sisi tuna hangaika sana na maneno ya wengine. Ni
vizuri kusikiliza wengine na kuwasiliana nao katika hali ya utambuzi. Mawazo ya
wengine yanaweza kuwa chanzo cha kugeukia maisha mazuri. Lakini wakati mwingine
tunaruhusu wengine watupeleke kwenye dhambi kwasababu ya hofu na woga. Wakati
mwingine mawazo mabaya na ushauri mbaya unaongoza maisha yetu. Yesu hakuingia
katika mawazo mabaya ya wengine wala hakuruhusu kupelekwa na kutenda kunyume.
Pili, Yesu hakuruhusu
“cheo” cha mtu kumpelekesha. Cheo cha mtu wala madaraka havi mfanyi mtu kuwa
mkweli zaidi kuliko wengine. Kilicho cha muhimu ni uaminifu na ukweli wa kila
mtu. Yesu alizitenda fadhila hizi kiaminifu.
Tutafakari pia sisi kama
maneno haya yanaweza kusemwa yakitulenga sisi. Tukazane kuishi maisha ya
unyenyenyekevu na kweli na hivyo tutavuka vikwazo na mitego iliyotegwa katika
njia yetu ya maisha.
Sala: Bwana, ninataka
kuwa mtu mwaminifu. Ninataka kusikiliza mawaidha mazuri ya wengine lakini sio
mawazo yakunipeleka kwenye dhambi. Nisaidie niweze kukutafuta wewe na ukweli
wako katika kila kitu. Yesu, nakuamini wewe. Amina.
------------------------
Copyright ©2013-2024
©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment