“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kwaresima
Jumamosi,
Febuari 21, 2021
Jumapili
baada ya Jumatano ya majivu
Mwa.
9:8– 15
1Pet:
3:18-22
Mk:
1: 12-15
Leo
ni Dominika ya Kwanza ya Kwaresima. Jumatano iliyopita wote tulikusanyika
katika liturujia ya Majivu na tukapakwa Majivu kama ishara ya toba tulipokianza
Kipindi hiki cha Kwaresima. Leo tunapaswa kutafakari zaidi juu ya toba yetu ya
kweli dhidi ya vishawishi vinavyotuzunguka katika ulimwengu huu. Liturujia ya
leo inatuonesha jinsi Yesu alivyopambana na vishawishi na alivyovishinda kwa
niaba yetu. Kumbe, kitupasacho sisi kwa sasa, ni kumsikiliza Yesu katika Neno
lake na hivi tushiriki ushindi wake.
Injili
ya leo, inaanza kwa kutuletea picha ya mchezo wa kuigiza. Pazia
linapofunguliwa, tutamwona Yesu yuko upande mmoja na Ibilisi upande wa pili.
Mara Ibilisi anamchukua Yesu na kumpeleka jangwani ili amjaribu huko. Lakini
ikumbukwe kuwa Yesu alikuwa amejazwa Roho Mtakatifu toka wakati wa Ubatizo wake
kule Yordani. Hivi alingia katika mapambano na Ibilisi akiwa amejazwa Roho Mtakatifu.
Mapambano yanayofanyika jangwani, yalimhusisha Yesu kukaa huko siku arobaini
akisali, kufunga na kujaribiwa. Baada ya siku hizo arobaini, Yesu anarudi
Galilaya, siyo kama mtu aliyechoka au kushindwa, bali kama mtu aliyejazwa Roho
Mtakatifu, na yuko tayari kuanza kazi ya ukombozi wa mwanadamu.
Leo
sisi tunaalikwa kuingia katika mapambano dhidi ya Ibilisi. Mungu anatutaka sisi
tukiwa pamoja na Kristo, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, kupambana na vishawishi
ambavyo vimo ndani yetu katika mazingira yetu, hatimaye tuvishinde vishawishi
hivyo. Ni suala la kila mkristo kujitoa mhanga katika kumfuata Roho wa Kristo
anayetuongoza jangwani.
Wito
huo wa Mungu unatufikia sisi kwa maneno yaleyale aliyosema Yesu alipoanza kazi
baada ya kurudi toka jangwani. Anasema: ‘Wakati umetimia na utawala wa Mungu
umekaribia. Tubuni na kuamini Injili.
Saa
ya neema
“Wakati
umetimia na utawala wa Mungu umekaribia”. Kila kitu kina wakati wake. Kitabu
cha Yoshua bin Sira kinatuambia: Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa
kufa...Wakati wa kulia na wakati wa kucheka..”. Na tunaweza kuongeza: ‘Wakati
wa kutubu’. Kuna wakati ambapo neema ya Mungu inamwingia mtu bila kutegemea.
Vivyo hivyo, uko wakati ambao Neno la Mungu linapenya moyoni mwa mtu na
kumgusa, na hivyo kumfanya abadilike. Hata katika historia ya Kanisa, tunapata
mifano ya watu ambao leo hii ni watakatifu wa na Neno la Mungu kwa wakati
fulani na hivyo wakabadilika.
Mtakatifu
Augustino wa Hippo, Margareta wa Kortona na wengine ni miongoni mwa watu hao.
Kumbe, kwetu sisi nasi, kipindi hiki ni kipindi cha neema, ni saa ya neema, ni
wakati wa kuguswa na Neno Ia Mungu na kubadilika.
Kutubu
na kuamini
Kuna
njia nyingi sana, na namna nyingi za kumwasi Mungu na kwenda kinyume na matakwa
ya Mungu. Lakini kumrudia Mungu iko njia moja tu. nayo ni ya kutubu na kuamini
juu ya uwezo wake wa kusamehe na kuponya dhambi. Unaweza ukajiona kuwa huna
dhambi na wala hujatenda dhambi kama yule jirani yako au rafiki yako, lakini
kumbuka kuwa unayo mapungufu yako na kasoro zako. Unayo mawazo na maneno
potofu. Hayo yote ni dharnbi mbele ya Mungu. Kipindi hiki ni kipindi cha kutubu
na kuamini juu ya uwezo wa Mungu wa kukusamehe hayo yote na kukuponya madhambi
yako.
Ndugu
zangu, kwaresima hii iwe nafasi nzuri ya kubadili mioyo yetu, fikra zetu, matendo
yetu tupate kumwelekea tuliyemwacha kutokana na maelekeo yetu mabaya. Pia iwe
nafasi nzuri ya kujipima jinsi gani tunamtegemea Mungu katika majaribu
mbalimbali ya kiroho na yale ya kimwili.
Tumwombe
Mungu basi, ili kwa njia ya Mwanae mteswa Yesu Kristo waitume zawadi yao kwetu,
yaani Roho Mt atupe nguvu na uwezo wa kuwa watu wa toba.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment