MASOMO
YA MISA, FEBRUARI 5, 2021
IJUMAA,
JUMA LA 4 LA MWAKA
KUMBUKUMBU
YA MT. AGATHA (MSHAHIDI)
SOMO
1
Ebr.
13:1 – 8
Upendano
wa ndugu na udumu. Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine
wamewakaribisha malaika pasipo kujua. Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba
mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mliavyo
katika mwili.
Ndoa
na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na
wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi
na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye ymwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa,
wala sitakuacha kabisa. Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye,
sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
Wakumbukeni
wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza
sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni Imani yao. Yesu Kristo ni yeye yule, jana
na leo na hata milele.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
27:1, 3, 5, 8 – 9 (K) 1
(K)
Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu.
Bwana
ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope
nani?
Bwana
ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu
nani? (K)
Jeshi
lijapojipanga kupigana nami,
Moyo
wangu hautaogopa.
Vita
vijaponitokea
Hata
hapo nitatumaini. (K)
Mradi
atanisitiri bandani mwake siku ya mabaya,
Atanisitiri
katika sitara ya hema yake,
Na
kuniinua juu ya mwamba. (K)
Bwana,
uso wako nitautafuta.
Usinifiche
uso wako,
Usijiepushe
na mtumishi wako kwa hasira.
Umekuwa
msaada wangu usinitupe. (K)
SHANGILIO
Zab.
130:5
Aleluya,
aleluya,
Roho
yangu inamngoja Bwana, na neno lake nimelitumainia.
Aleluya.
INJILI
Mk.
6:14-29
Mfalme
Herode alisikia habari; kwa maana jina lake lilikuwa kutangaa, akasema, Yohane
Mbatizaji amefufuka katika wafu, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani
yake. Wengine walisema, Ni Eliya. Wengine walisema, Huyu ni nabii, au ni kama
mmoja wa manabii. Lakini Herode aliposikia, alisema, Yohane mwenyewe alikuwa
amefufuka.
Kwa
maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma watu, akamkamata Yohane, akamfunga
gerezani, kwa ajili ya Herodia, mkewe Filipo ndugu yake; kwa kuwa amemwoa; kwa
sababu Yohane alimwambia Herode, Si halali kwako kuwa na mke wa nduguyo. Naye
yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asipate. Maana Herode alimwogopa
Yohane; akimjua kuwa ni mtu wa haki, mtakatifu, akamlinda; na alipokwisha
kumsikiliza alifadhaika sana; naye alikuwa akimsikiliza kwa furaha.
Hata
ilipotokea siku ya kufaa, na Herode, sikukuu ya kuzaliwa kwake, alipowafanyia
karamu wakubwa wake, na majemadari, na watu wenye cheo wa Galilaya; ndipo binti
yake yule Herodia alipoingia, akacheza, akampendeza Herode na wale walioketi
pamoja naye karamuni. Mfalme akamwambia yule kijana, Niombe lolote utakalo
nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu. Basi akatoka, akamwuliza mamaye, Niombe
nini? Naye akasema, Kichwa cha Yohane Mbatizaji. Mara akaingia kwa haraka mbele
ya mfalme, akaomba akisema, Nataka unipe sasa hivi katika kombe kichwa cha
Yohane Mbatizaji.
Mfalme
akafanya huzuni sana, lakini kwa ajili ya viapo vyake, na kwa ajili ya hao
walioketi karamuni, hakutaka kumkatalia. Mara mfalme akatuma askari, akaamuru
kuleta kichwa chake. Basi, akaenda, akamkata kichwa mle gerezani, akakileta
kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye.
Wanafunzi
wake waliposikia habari, walikwenda, wakauchukua mwili wake, wakauzika
kaburini.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment