MASOMO
YA MISA, FEBRUARI, 27, 2021
JUMAMOSI,
JUMA LA 1 LA KWARESIMA
SOMO
1
Kumb.
26:16-19
Musa
aliwaambia watu: Leo hivi akuamuru Bwana, Mungu wako, kuzifanya amri hizi na
hukumu; basi uzishike na kuzifanya kwa moyo wako wote na roho yako yote.
Umemwungama
Bwana leo, kuwa ndiye Mungu wako, na kuwa yakupasa kutembea katika njia zake,
na kushika amri zake na maagizo yake, na hukumu zake, na kusikiza sauti yake;
naye Bwana amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama
alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote; na kuwa atakutukuza
juu ya mataifa yote aliyoyafanya kwa sifa, na jina na heshima, nawe upate kuwa
taifa takatifu kwa Bwana Mungu wako, kama alivyosema.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
119:1-2, 4-5, 7-8
(K)
Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya Bwana.
Heri
walio kamili njia zao,
Waendao
katika sheria ya Bwana.
Heri
wazitiio shuhuda zake,
Wamtafutao
kwa moyo wote. (K)
Wewe
umetuamuru mausia yako,
Ili
sisi tuyatii sana.
Ningependa
njia zangu ziwe thabiti,
Nizitii
amri zako. (K)
Nitakushukuru
kwa unyofu wa moyo,
Nikiisha
kujifunza hukumu za haki yako.
Nitazitii
amri zako,
Usiniache
kabisa. (K)
SHANGILIO
Amo.
5:14
Tafuteni
mema, wala si mabaya, mpate kuishi, hivyo Bwana, atakuwa pamoja nanyi.
INJILI
Mt.
5:43-48
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake: Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na,
Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni
wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yetu aliye mbinguni; maana yeye
huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu? Hata watoza ushuru; je!
Nao hawafanyi yay ohayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la
ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa
wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment