“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumatatu,
Februari 8, 2021.
Juma
la 5 la Mwaka
Mwanzo
1: 1-19;
Zab
104: 1-2, 5-6, 10, 12, 24, 35;
Mk
6: 53-56.
KUKIMBILIA
KWA YESU
Karibuni
ndugu zangu kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Neno la Bwana leo
linatueleza kwamba Mwenyezi Mungu anaupenda ulimwengu, yeye ndiye aliyeuumba
ulimwengu kwa nguvu ya neno lake, akapanga majira yote. Ndiye aliyeumba mito na
vijito vyote. Dunia inapendeza kwa sababu yake. Tunamuomba azidi kuulinda ulimwengu
wote.
Changamoto
iliyopo ni mwanadamu kuharibu uumbaji na kwa ujanja ujanja wake. Anaingiza vitu
visivyokuwa katika mpango wa Mungu. Anataka alete hata ndoa za jinsia moja.
Anataka kuingiza hata matunda yanayozalishwa na kemikali na kupata ukubwa wa
ajabu. Anacheza na uumbaji na kuzalisha vitu vya haraka haraka, kuku wa haraka
haraka lakini vyote hivi vinauteketeza ulimwengu. Baadhi ya wanaume wameota
matiti kutokana na kemikali zinazozalishwa na huyu mwanadamu anayeingilia
uumbaji. Anadiriki hata kutengeneza mvua. Haya yote ni uchu wa mwanadamu kutaka
kupata mali nyingi bila kujali afya ya wengine Uumaji wa Mungu tunauharibu.
Tumwombe Mungu atufundishe kuutunza ulimwengu wake. Pia tumuombe atazame zile
sehemu zinazotawaliwa na ukame na uchafu aziangalie kwa namna ya pekee.
Katika
injili yetu, Yesu anawaponya wagonjwa mbalimbali. Injili ya leo inatuambia
kwamba ni wale waliomgusa ndio tu walioponywa. Hivyo tukitaka uponyaji toka kwa
Yesu, ni lazima tunyanyuke na kumgusa Yesu. Tusilale tukitegemea kuna
atakayemgusa kwa ajili yetu. Tunyanyuke sisi wenyewe na kumgusa. Hata ukija
kanisani, yabidi kunyanyuka sisi kama sisi na kumgusa, tusitegemee kwamba kuna
anayemgusa kwa ajili yako. Kila mtu anakuja na shida yake. Hivyo lazima nimguse
kwa namna ya pekee, nikutane naye. Usilale na kusema Mama/Baba au rafiki
anasali kwa niaba yangu.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment