MASOMO
YA MISA, JANUARI 8, 2021
IJUMAA
BAADA YA EPIFANIA
SOMO
1
1Yoh.
5:5-6, 8-13
Wapenzi:
Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu
ni Mwana wa Mungu? Huyu ndiye aliyekuja kwa maji wa damu, Yesu Kristo; si
katika maji tu, bali katika maji na katika damu. Kwamaana wako watatu
washuhudiao (mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni
umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani), Roho, na maji, na damu; na
watatu hawa hupatana kwa habari moja.
Tukiupokea
ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa
Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu
anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa
kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe. Na huu ndio
ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika
Mwanawe. Yeye aliye naye Mwana, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana
huo uzima. Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa
milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
147:12-15, 19-20 (K) 12
(K)
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu.
Msifu
Bwana, Ee Yerusalemu;
Msifu
Mungu wako, Ee Sayuni.
Maana
ameyakaza mapingo ya malango yako,
Amewabariki
wanao ndani yako. (K)
Ndiye
afanyaye amani mipakani mwako,
Akushibishaye
kwa unono wa ngano.
Huipeleka
amri yake juu ya nchi;
Neno
lake lapiga mbio sana. (K)
Humhubiri
Yakobo neno lake,
Na
Israeli amri zake na hukumu zake.
Hakulitendea
taifa lolote mambo kama hayo,
Wala
hukumu zake hawakuzijua. (K)
SHANGILIO
1Tim.
3:16
Aleluya,
aleluya,
Sifa
kwako, Ee Kristo, uliyehubiriwa katika mataifa; Sifa kwako, Ee Kristo,
aliyeaminiwa katika ulimwengu.
Aleluya.
INJILI
Lk.
5:12-16
Ikawa
Yesu alipokuwa katika mmojawapo wa miji ile, tazama, palikuwa na mtu amejaa
ukoma; naye alipomwona Yesu alianguka kifudifudi, akamwomba akisema, Bwana,
ukitaka, waweza kunitakasa. Naye akaunyosha mkono wake, akamgusa akisema,
Nataka; takasika. Na mara ukoma wake ukamwondoka. Akamkataza asimwambie mtu,
ila, Nenda ukajionyeshe kwa kuhani; ukatoe kwa ajili ya kutakasika kwako kama
Musa alivyoamuru, iwe ushuhuda kwao.
Lakini
habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na
kuponywa magonjwa yao. Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa
na watu, akaomba.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment