MASOMO
YA MISA, JANUARI 5, 2021
JUMANNE
BAADA YA EPIFANIA
SOMO
1
1Yoh.
4:7-10
Wapenzi,
tupendani; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na
Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni
upendo. Katika hili pendo la Mungu lilionekana kwetu, kwamba Mungu amemtuma
Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. Hili ndilo pendo, si
kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma
Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
72:1-2,10,12-13 (K) 11
(K)
Mataifa yote ya ulimwengu, watakusujudia, Ee Bwana.
Ee
Mungu, mpe mfalme hukumu zako.
Na
mwana wa mfalme haki yako.
Atawaamua
watu wako kwa haki,
Na
watu wako walioonewa kwa hukumu. (K)
Milima
itawazalia watu amani,
Na
vilima navyo kwa haki.
Atawahukumu
walioonewa wa watu,
Atawaokoa
wahitaji, atamseta mwenye kuonea. (K)
Siku
zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi,
Na
wingi wa Amani hata mwezi utakapokoma
Na
awe na enzi toka bahari hata bahari,
Toka
mto hata miisho ya dunia. (K)
SHANGILIO
Aleluya,
aleluya,
Naye
Yesu alikuwa akihubiri Habari njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa
kila namna katika watu.
Aleluya.
INJILI
Mk.
6:34-44
Siku
ile, Yesu aliona mkutano mkuu, akawahurumia; kwa sababu walikuwa kama kondoo
wasio na mchungaji; akaanza kuwafundisha mambo mengi.
Hata
zilipopita saa nyingi za mchana, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali
hapa ni nyika tupu, na sasa kunakuchwa; uwaage watu hawa, ili waende zao
mashambani na vijijini kandokando, wakajinunulie chakula. Akajibu, akawaambia,
Wapeni ninyi chakula. Wakamwambia, Je! Twende tukanunue mikate ya dinari mia
mbili ili tuwape kula? Akawaambia, Mnayo mikate mingapi? Nendeni mkatazame.
Walipokwisha kujua wakasema, Mitano, na samaki wawili.
Akawaagiza
wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabichi. Wakaketi safu safu, hapa
mia hapa hamsini. Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama
mbinguni, akashukuru, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake wawaandikie;
na wale samaki wawili akawagawia wote. Wakala wote wakashiba. Wakaokota vipande
vilivyomegwa vya kuweza kujaza vikapu kumi na viwili; na vipande vya samaki
pia. Na walioila ile mikate wapata elfu tano wanaume.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment