MASOMO
YA MISA, JANUARI 15, 2020
IJUMAA,
JUMA LA 1 LA MWAKA
SOMO
1
Ebr.
4:1 – 5, 11
Ikiwa
ikaliko ahadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije
akaonekana ameikosa. Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa habari njema vile
vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu
halikuchanganyika na Imani ndani yao waliosikia. Maana sisi tulioamini
tunaingia katika raha ile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira
yangu, hawataingia rahani mwangu; ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu
kuwekwa misingi ya ulimwengu. Kwa maana ameinena siku ya saba mahali Fulani
hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; na hapo napo,
Hawataingia rahani mwangu.
Basi,
na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka
kwa mfano huo huo wa kuasi.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
78:3 – 4, 6 – 8 (K) 7
(K)
Msiyasahau matendo ya Mungu.
Mambo
tuliyoyasikia na kuyafahamu,
Ambayo
baba zetu walituambia,
Tukiwaambia
kizazi kingine
Sifa
za Bwana na nguvu zake. (K)
Wasimame
na kuwaambia wana wao,
Wamwekee
Mungu tumaini lao,
Wala
wasiyasahau matendo ya Mungu,
Bali
wazishike amri zake. (K)
Wasiwe
kama baba zao,
Kizazi
cha ukaidi na uasi,
Kizazi
kisichojitengeneza moyo,
Wala
roho yake haikuwa amini kwa Mungu. (K)
SHANGILIO
Yn.
17:17
Aleluya,
aleluya,
Neno
lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.
INJILI
Mk.
2:1-12
Baada
ya siku Yesu akaingia tena Kapernaumu. Ikasikiwa ya kwamba Yesu alikuwa
nyumbani. Wakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema
nao neno lake. Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu
wanne. Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa
dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia
yule mwenye kupooza.
Naye
Yesu, alipoiona Imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu,
umesamehewa dhambi zako. Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi,
wakifikiri mioyoni mwao, Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye
kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?
Mara
Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia,
Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu? Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza,
Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende? Lakini
mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi,
(hapo amwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako,
uende nyumbani kwako. Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao
wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata
kuiona kamwe.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment