“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumapili,
Januari 31, 2021,
Juma
la 4 la Mwaka wa Kanisa
Kum
18:15-20
1
Kor 7: 32-35
Lk
1: 69-75;
Mkc1:
21-28
Watu
tunaishi katika mazingira mbali mbali na hivi kutofautiana kimaisha. Wengine
wagonjwa, wengine wazima, dhaifu, maskini na fukara. Hata hivyo, ubatizo
unatuunganisha, wote tunakuwa kitu kimoja. Yaani, kila mmoja wetu amepewa
nafasi ya pekee ya kueneza Injili kadiri ya hali yake.
Kum
18:15-20
Nabii
anaonesha mamlaka yake, pale anapoutangaza ujumbe wa Mungu, kwa watu kiaminifu,
na maneno yake yanabeba ujumbe wa Mungu. Kama nabii, akianza kuhubiri ujumbe au
mawazo yake binafsi, huo unakuwa si unabii, bali anakuwa hana tofauti na mtu
yeyote anayeongea mambo ya kawaida.
Katika
Agano la Kale alikuwa Musa na manabii wengine. Katika Agano Jipya walikuwa
mitume ambao baada ya kumpokea Roho Mtakatifu siku ya Pentekoste walitangaza
Habari Njema kwa bidii yote. Sasa kazi hiyo hufanywa na jumuiya yote ya wakristo.
Sisi sote ni manabii kwa kuisikiliza sauti ye Mungu na kuisambaza popote
ulimwenguni. Kwa kuwa tu manabii hasa kwa njia ya ubatizo wetu, tunapaswa
kuangalia hali halisi ya watu, familia na taifa ndipo tulete mwanga wa Habari
Njema kwao.
Katika
injili ya leo tunajifunza kuwa, Yesu anafundisha kama mtu mwenye mamlaka ya
pekee. Ni tofauti kabisa na Waandishi ambao walitoa mafundisho yasiyo yao. Wao
walinukuu mafundisho ya watu wao. Lakini Yesu alifundisha kwa njia tofauti.
Yeye alitumia mamlaka yake mwenyewe. Alizungumza kwa uhuru wote. Alizungumza
kadiri ya sauti ya Mungu ilivyomwongoza.
Watu
waliokuwa tayari kumsikiliza Yesu walipata faraja sana, kwani maneno yake
yaligusa mioyo yao. Ndiyo kusema, ujumbe wenye mamlaka toka kwa mtu mwenyewe,
una nguvu ya pekee ya kuvuta watu waweze kumsikiliza.
Yesu
aliwapa watu ujumbe wa Mungu. Ujumbe huo ulikuwa ni maisha yake yeye mwenyewe.
Watu walionja kuwa Yesu alizungumza kile alichoamini na kuona kuwa ni cha
kweli. Alifundisha kile ambacho yeye mwenyewe alikiishi.
Najiuliza
mwenyewe, Je, ninapozungumzia habari za Mungu, au za kanisa, kweli ninayaamini
hayo nisemayo? Tumesikia kuwa, baada ya Yesu kutoa mafundisho, mtu mwenye pepo
mchafu alitokea ndani ya sinagogi.
Nyakati
zile za yesu, haukuwepo utaalam wa kisayansi kuhusu madawa, bakteria, kifafa au
ugonjwa wa akili. Yeyote aliyepatwa na matatizo ya kiafya yanayohusiana na
akili, alidhaniwa kuwa ana pepo wachafu. Kadiri ya imani ya Wayahudi waliamini
kuwa pepo wachafu walitoka baharini, angani, na kwenye makaburi. Hakuna
aliyekuwa na uhakika kamili kwamba wapi hao pepo wachafu walitoka.
Mtu
mwenye pepo mchafu ni yule anayepingana na utakatifu wa Mungu. Pepo huyo
humtesa binadamu na humzuia asiwe katika ubinadamu wake halisi. Mtu anayeteswa
na pepo mbaya anakuwa kama mtu aliyetengwa. yuko uhamishoni, anakosa amani na
hana furaha.
Vilevile,
aliyepagawa na pepo mchafu, anakuwa bado hajakutana na Kristo. Anakuwa na nguvu
za giza kama vile za ubaguzi wa rangi, ukabila, imani za ushirikina, ulevi,
ubinafsi n.k.
Kulikuwa
na mapambano makali kati ya Yesu na huyo aliyepagawa na pepo, kwani mtu mwenye
tabia za hapo juu hapendi kuacha tabia zake hizo chafu.
Yesu
amekuja kumkomboa mwanada mu kutoka katika nguvu zile zina zomfanya asiwe huru,
aonekane amete ngwa na yuko uhamishoni. Kama wakristo tunapaswa kutambua kuwa
tuko vitani pamoja na Kristo. Mkristu aliyejiweka mikononi mwa Yesu Kristo,
ataushinda uovu, na kumshinda mwovu. Anapaswa atambue ni uovu gani anaopambana
nao kila siku ambao humfanya ajione hayuko huru, au uovu unao wafanya wengine
wasiwe huru, la mateka.
Tuwe
wakweli mahali ambapo pamejaa uovu. Tena, tuyaishi yale ambayo tunayahubiri kwa
watu iii wao watuone kuwa kweli sisi ni wakristo.
Tukutanapo
na mtu asiyelijua Neno a Mungu kutokana na jinsi anavyoishi, tumwelimishe,
tusikubali kushindwa eti kwa sababu ya woga kwa kuwa moyo wake umekuwa mgumu,
bali tuwe wavumilivu mpaka hapo atakapopata mwanga wa Kristo.
Tunaalikwa
leo pia kuwaombea kwa namna ya pekee wale ambao wanafanya kazi ya kulitangaza
Neno Ia Mungu, hasa makatekista, mapadri, maaskofu na watawa.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment