“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba 19, 2020.
------------------------------------------------
JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA MAJILIO
Somo la 1: Amu 13: 2-7, 24-25 Samson
anachukuliwa mimba kimiujiza. Anaongozwa na Roho Mtakatifu na Mungu amekusudia
kumtumia kwa ajili ya mpango wa watu wake.
Wimbo wa katikati : Zab 70: 3-6, 16-17 ni
wewe, Ee Bwana uliye tumaini langu, ninayekuamini, Ee Bwna kutoka kwako
nimejifunza tangu kuzaliwa kwangu, tangu tumboni mwa Mama yangu umekuwa msaada
wangu.
Injili: Lk 1: 5-25 Luka anahusisha
simulizi la tangazo la Malaika kwa Zakaria kwamba Elizabeth mke wake ambaye
hakuwa na mtoto atazaa mtoto na jina lake ataitwa Yohane.
------------------------------------------------
YANAWEZEKANAJE HAYA?
Inavutia kulinganisha mazungumzo kati ya
Zakaria na Malaika Gabriel na yale ya Maria na Malaika Gabriel. Majibu yao kwa
malaika Gabrieli yanaonekana kuwa sawa, lakini Malaika Gabrieli anaonekana
kumjibu kila mtu kitofauti kabisa. Kwa Maria, malika Gabrieli anaelezea maelezo
machache, baada ya ombi la Maria la kutaka maelezo: “Hili linawezekanaje” Maria
alisema. Gabriel anajibu “Roho Mtakatifu atakufunika …..” lakini katika hali
hii kwa Zakaria hakutoa maelezo. Na badala yake Zakaria anakuwa bubu kwasababu
ya kushindwa kuamini. Ingawaje majibu ya Maria na Zakaria yanaweza kuonekana
kama yanafanana kwa kuangalia tu katika hali ya kawaida, ni Dhahiri kwamba
mioyo yao ilikuwa tofauti. Kwa Maria Mama Mbarikiwa, swali lake aliliuliza
katika Imani kamilifu. Alisikia Gabrieli akiongea akaamini. Lakini Imani huwa
inatafuta kuelewa, na ndivyo kwa Maria katika Imani timilifu, alitafuta kuelewa
fumbo ambalo linakuja kwake. Malaika Gabrieli anajibu kwa kumweleza kwa kifupi,
na Maria anafurahi kwa hilo..
Zakaria alimjibu Malaika, “nitajuaje
hili?” kwa maneno mengine, anakiri kutoelewa kama maneno haya yatakuwa kweli.
Hivyo alikuwa bubu, alama ya kwamba, kama huna Imani, hakuna chakusema.
Kila wakati Mungu anapojifunua kwetu,
tunapaswa kwanza kuamini, na kwa unyenyekevu mkubwa, tutafute ufafanuzi.
Tufikirie juu ya Imani yetu. Je, tupo tayari kutaka kuelewa na kukubali yote
anayotaka kutufunulia Mungu? Je, tupo tayari kukubali na kuamini anayo ongeo
Mungu juu yetu? Ingawaje mimi na wewe pengine hatupokei tena neno lake moja kwa
moja kupitia kwa malaika kwa kumuona kwa macho, tuna bahati ya kuwa na Mungu
akiongea nasi kwa njia ya Neno lake. Je, tunasikiliza na kujibu kwa Imani kama Mama
yetu Maria au Zakaria.
Sala: Bwana, ninaomba unipe moyo na Imani
kama ya Mama Bikira maria Mtakatifu. Japo, nakubali juu ya udhaifu wangu na
dhambi zangu, ninaomba kwa mfano wake na maombezi yake, nipokee kila siku neno
lako linalo hubiriwa kwetu. Ninaomba kila wakati niwe makini kwa neno lako na
kulipokea kwa moyo wa ukarimu. Yesu nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright ©2013-2020 ©FurKat,
FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment