“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba
7, 2020.
Jumatatu,
JUMA LA 2 LA MAJILIO
Somo
la 1: Isa 35:1-10 Isaya anatoa picha ya “nyakati za Masiha” ni katika uzuri wa
jangwa linalo furahi na ubinadamu ulioponywa kutoka katika magonywa yote.
Wimbo
wa katikati: Zab 85: 9-14 tazama, Mungu anakuja kutukomboa. Haki itamtangulia
yeye….na Amani itafuata hatua zake.
Injili:
Lk 5: 17-26 Sisi tunafanywa hai kiroho na kimwili kama yule aliyepooza. Yesu
anathibitisha kwamba anauwezo wakusamehe dhambi kwa njia ya muujiza wa kuponya.
------------------------------------------------
TAMAA
YA KUTAKA KUPONYWA NA KUSAMEHEWA
Katika
somo la kwanza, nabii Isaya anatangaza ujio wa zama za Kimasiha ambao wale
walio wanyonge, viwete, watafurahi, yaani maeneo yote yasio na matumaini,
yatafurahi. Ujio wa Yesu ulizitimiza hizi zama. Nchi ilipata kufurahi na jangwa
na palipo na ukiwa pakawa na furaha. Vilema waliruka ruka, bubu wakaongea,
viziwi wakasikia, wenye njaa kupewa chakula na maskini kuhubiriwa habari njema.
Hapa kwa kweli alitimiza zile zama za Kimasiha. Aliwaondolea watu vifungo
vikubwa vya dhambi, vilivyoyafanya maisha yao na miili yao ipooze kama
anavyomwondolea huyu mgonjwa anayemponya leo.
Hapa
alimaanisha kwamba dhambi ni mbaya, haizoeleki, kwa sababu inafanya maisha ya
mtu yapooze, yaparalyze, inaifanya jamii iparalyze. Hivyo isiachwe bila
kukemewa. Kwa kufanya hivi, Yesu alituachia majukumu sisi wafuasi wake kwamba
lazima tuendelee kuzitangaza zama hizi. Kutangaza zama za Kimasiha yamaanisha
kwamba dhambi haivumiliwi, usione dhambi ushindwe kuikemea. Usione uovu
unaendelea kutendeka wewe ukae kimya au ujiunge nao. Uovu huipoozesha roho,
huparalyze maisha ya kiroho ya mkristo mwenyewe na jamii nzima. Na katika
kitabu cha ufunuo, huu ujumbe unafanana na ule alioutoa Roho kwa kanisa ya
Thiatira. Kanisa hili lilivumilia dhambi, lilishindwa kuwakemea wale wakristo
MAARUFU, likavumilia dhambi zao na mwishowe wakaelekea kulibomoa kabisa. Roho
aliliambia hili kanisa kwamba lisipotubu na kuwakemea hawa, litateketezwa na yule
ambaye macho yake ni moto, akiangalia kitu-kiovu kinateketea chote. Hivyo, kama
watu tunaotangaza zama za Kimasiha, tusiache hata siku moja kuikemea dhambi.
Kemea uovu, uovu huteketeza jamii yote.
Penye
kosa sema hapa pana kosa, usingate na kupuliza, hata kama ni maskini, hata kama
ni mdogo mwambie umekosea, hata kama ni mtoto wako anayekupaga mchango mkubwa
sana, akikosea mwambie hapa umekosea. Usipofanya hivyo jua unayapoozesha maisha
yake na hata yako na baadaye ya jamii nzima.
Hata
kama ni rafiki yako wa karibu-kama kakosea mwambie kakosea, mwambie hapa
umechemka. Huu ndio ukristo. Hii kutafuta tafuta urafiki hapa, haiendi jamani,
haiendi jamani. Tuombe nguvu kutoka kwa Yesu tuweze kutimiza hili kwa Imani kuu
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment