MASOMO YA MISA,
JUMATANO, DESEMBA 23, 2020
JUMA LA 4 LA MAJILIO
SOMO 1
Mal. 3:1 – 4; 4:5 – 6
Bwana Mungu asema: Angalieni, namtuma
mjumbe wangu, naye ataitengeneza njia mbele yangu; naye Bwana mnayemtafuta
atalijilia hekalu lake ghafula; naam, yule mjumbe wa agano mnayemfurahia,
angalieni, anakuja, asema Bwana wa majeshi. Lakini ni nani atakayestahimili
siku ya kuja kwake? Kwa maana yeye ni mfano wa moto wa mtu asafishaye fedha, ni
mfano wa sabuni ya mtu afuaye nguo; naye ataketi kama asafishaye fkama asafishaye
fedha na kuitakasa, naye atawatakasa wana wa Lawi, atawasafisha kama dhahabu na
fedha; nao watamtolewa Bwana dhabihu katika haki. Wakati ule ndipo dhabihu za
Yuda na Yerusalemu zitakapopendeza mbele za Bwana, kama katika siku za kale, na
kama katika miaka ya zamani.
Angalieni, nitawapelekea Eliya nabii,
kabla haijaja siku ile ya Bwana, iliyo kuu na kuogofya. Naye ataigeuza mioyo ya
baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ioli nisije
nikaipiga dunia kwa laana.
Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 25:4 – 5, 8 – 10, 14
(K) Changamkeni, mkaviinue vichwa vyenu,
kwa kuwa ukombozi wenu unakaribia.
Ee Bwana, unijulishe njia zako,
Unifundishe mapito yako.
Uniongoze katika kweli yako,
Na kunifundisha.
Maana wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu.
(K)
Bwana yu mwema, mwenye adili,
Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.
Wenye upole atawaongoza katika hukumu,
Wenye upole atawafundisha njia yake. (K)
Njia zote za Bwana ni fadhili na kweli,
Kwao walishikao agano lake na shuhuda
zake.
Siri ya Bwana iko kwao wamchao,
Naye atawajulisha agano lake. (K)
SHANGILIO
Aleluya, aleluya,
Ee Imanueli, Mfalme na Mwanasheria wetu,
njoo ukatuokoe, ee Bwana, Mungu wetu.
Aleluya.
INJILI
Lk. 1:57 – 66
Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti
zilipotimia alizaa mtoto mwanamume. Wakasikia jirani zake na jamaa zake,
wakafurahi pamoja naye.
Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto
wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamayeakajibu akasema, La, sivyo; bali,
ataitwa Yohani. Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zake aitwaye jina hilo.
Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita. Akataka kibao, akaandika kwamba,
Jina lake ni yohane. Wakastaajabu wote. Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na
ulimi wake pia, akaanza kunena akimsifu Mungu.
Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa
karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima milima
ya Uyahudi. Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu
atakuwa wa namna gani. Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.
Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.
-------------------------
Copyright © 2020, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment