“ASALI
MUBASHARA”
Januari
5, 2021.
------------------
Jumanne,
baada ya Epifania
1
Yn 4: 7-10;
Zab
72: 1-4, 7-8;
Mk
6: 34-44.
KUTAMANI
UTAKATIFU!
Ndugu
zangu wapendwa karibuni kwa adhimisho la Misa Takatifu asubuhi ya leo. Yesu
katika injili anakutana na makutano ya watu, wanaotangatanga na kuangalia kama
kondoo wasio na mchungaji.
Kondoo
asiye na mchungaji mara nyingi huishia kula takataka kwa kukosa mchungaji wa
kuwaongoza. Halafu hajui aendako na mara nyingi hupotea kirahisi au kuliwa na
wanyama wakali.
Yesu
aliwaona makutano wakiwa katika hali hii. Walikabiliwa na vitu kama magonjwa,
njaa, ukosefu wa imani na maarifa. Yote haya yangewasababishia kuishia kutekwa
na ushirikina, uregevu, na imani potofu. Lakini Yesu aliamua kuingilia kati na
kuwalisha neno na kuwaongoza.
Sisi
kila mara tupo na kondoo wasio na mchungaji. Tupo na mayatima lakini wanaishia
kuwa chokoraa mtaani, wapo wagonjwa waliokata tamaa na kuishia kwenye
ushirikina. Yote haya yanatuhimiza tujitolee, tuchukue nafasi ya uchungaji.
Tukikutana na yatima waliotelekezwa tuchukue nafasi ya uchungaji. Tukikutana na
familia iliyojaa uregevu basi tuchukue nafasi ya uchungaji. Imani yetu yahimiza
tujitolee zaidi.
Tuongeze
majitoleo. Bila majitoleo ama kweli injili ya Bwana itashindwa kusonga mbele.
Somo
la kwanza linatusisitizia tuwe na upendo. Upendo wadai majitoleo. Yesu
alijitolea na kwa majitoleo hayo, sisi sote tumeweza kupewa uzima. Sisi
tujitolee ili na wenzetu wapate uzima. Wengi wanapoteza uhai kutokana na
kukosekana kwa wanaojitolea. Tuiokoe dunia kwa kuongeza idadi ya wanaojitolea.
Tuanze sasa, kwa majitoleo yetu wenyewe dunia itapata baraka na nafuu.
Tumsifu
Yesu Kristo.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment