“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Desemba
8, 2020.
------------------------------------------------
JUMANNE,
JUMA LA 1 LA MAJILIO
Sherehe
ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili.
Somo
la 1: Mwa 3:9-15, 20 wakati mwanamke na mwanamume walivYo acha kumtii Mungu na
kuanguka kwenye dhambi, Mungu alihidi ukombozi kutoka kwenye dhambi, kwa njia
njia nyingine kwa kupitia Maria na Kristo.
Wimbo
wa Katikati: Zab 97:1-4 Mungu ameunda ukombozi wake. Miisho yote ya ulimwengu
imeuona wokovu wa Mungu wetu.
Somo
la Pili 2: Ef 1:3-6, 11-12 kwa upendo wake kwetu, Mungu ametufanya sisi wanae.
Na hivyo tumeitwa kwenye utakatifu na maisha yasio na mawaa.
Injili:
Lk 1:26-38 Ukuu wa Maria na utakatifu wake ni kwasababu ya neema ya Mungu na
kushirikiana na hiyo neema.
------------------------------------------------
DHAHABU
SAFI
Leo
tuna adhimisha sherehe ya Bikira Maria mkingiwa dhambi ya asili. Maria ni
Mkingiwa Dhambi ya Asili: Somo la kwanza laezea jinsi dhambi ya asili
ilivyoingia ulimwenguni. Ilisababishwa na ukosefu wa utii wa mwanadamu kwa kula
tunda la mti uliokatazwa. Dhambi hii ni chanzo cha kifo, kutokuaminiana, hofu
baina ya viumbe pamoja na dhiki. Binadamu wote hurithi dhambi hii mara
wanapozaliwa lakini Bikira Maria alikingwa asipate dhambi hii. Mungu mwenyewe
ndiye aliyemkinga na dhambi hii ili akawe kikao kitakatifu cha mwanae.
Ukweli
huu unadhihirika katika injili ya leo pale malaika anapomsalimia Maria kwa
maneno kwamba ni mwingi wa neema. Hii yamaanisha kukosekana kwa doa lolote la
dhambi kwa Bikira Maria na mtoto atakayemzaa hatakuwa pia na doa lolote la
dhambi. Miili ya wote wawili, Mama na mtoto haikuoza kaburini. Yesu alipaa
mbinguni mwili na Roho na Maria alipalizwa mbinguni mwili na Roho (Katekisimu
ya Kanisa Katoliki 966). Hivyo, tusiogope kuomba kupitia maombi ya Mama Maria
sisi tuliozaliwa na dhambi ya asili. Yeye aliiletea dunia neema. Yeye
atatugawia neema alizopewa na Mungu na pia atatupeleka kwa Yesu mwanae.
Tumwombe tukisema, Ee Maria uliyekingiwa dhambi ya Asili utuombee sisi tunaozaliwa
na dhambi ya Asili! Amina!
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment