“ASALI ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kila siku
Jumatatu,
Novemba 23, 2020.
Juma
la 34 la Mwaka
Uf
14: 1-5;
Zab
24: 1-6
Lk
21: 1-4.
MOYO
WA UKARIMU!
Leo
Yesu anaona wema na ukarimu wa mama mjane, hakuhitaji kujitangaza au kutangaza
alichokuwa anafanya, na huenda pia alikuwa na aibu juu ya wale matajiri, ambao
walitoa kwa wingi wa vitu, na kuwafanya watu wengine watamani uhuru wao. Lakini
Mama huyu katika moyo wake usiojaa majivuno, alitoa kile alichokuwa nacho kama
sadaka yake, na anasatahili sifa alizotoa Kristo. Alitoa kila kitu alichokuwa
nacho kwani alikuwa na Mungu ndani ya moyo wake. Ni vizuri sana kuwa na Mungu
ndani ya mioyo yetu kuliko kuwa na dhahabu katika makabati yetu.
Tazama
baadhi ya watakatifu wengi walioishi bila kujionesha. Mfano Mt. Thérèsa wa
Lisieux, alijotoa kwa Kristo katika hali ya vitu vidogo. Aliishi ndani ya
nyumba yao ya kitawa kwa muda bila hata ya kuhangaika na malimwengu. Kwahiyo
katika mtazamo wa ulimwengu anaonekana amechangia kidogo sana katika ulimwengu.
Lakini leo hii ni Mwalimu wa Kanisa tunashukuru kwa zawadi ya maisha yake ya
kiroho na ushuhuda wa maisha yake.
Yanaweza
yakasemwa haya kwako pia. Pengine unajihangaisha na kitu ambacho ulimwengu
unaona hakina thamani. Pengine, kupika, kuosha vyombo na kuhudumia familia na
shughuli za kila siku. Swali la kujiuliza ni Mungu ananiona je?, sio ulimwengu
unanionaje.
Tafakari
leo juu ya maisha yako. Pengine hujaitwa ili uende ukafanyea mambo makubwa
katika hali ya kuonekana na watu au katika hali ya Ulimwengu. Au pengine
haukufanya kitu kikubwa kinacho onekana katika kanisa. Lakini anacho ona Mungu
ni ule upendo wako unaonekana katika mambo hayo madogo unayotenda kutimiza
majukumu yako ya kila siku, kuwapenda familia yako, kusali kila siku nk, ni
baadhi ya sadaka unayompa Mungu kila siku. Anaona hili na muhimu kabisa, anaona
upendo na majitoleo ambayo unayofanya. Fanya mambo hayo madogo kwa upendo
mkubwa na utakuwa ukimpa Mungu mengi kabisa katika kutimiza mapenzi yake.
Sala:
Bwana, ninajitoa mimi mwenyewe kwako na kwa huduma yako kila siku. Ninaomba
nifanye yanayo nipasa kutenda kwa upendo mkubwa. Ninaomba uendelee kunionesha
mimi majukumu yangu na ninaomba unisaidie mimi niweze kujikita katika majukumu
hayo kadiri ya mapenzi yako matakatifu. Bwana Yesu nakuamini wewe. Amina
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment