MASOMO YA MISA, NOVEMBA 28, 2020
JUMAMOSI,
JUMA LA 34 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Ufu.
22:1 – 7
Malaika
alinionyesha, mimi Yohane, mto wa maji ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri,
aukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwanakondoo, katikati ya njia
kuu yake. Na upande huu na upande huu wa ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao
matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya
mti huo ni ya kuwaponya mataifa. Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Na kiti
cha enzi cha Mungu na cha Mwanakondoo kitakuwamo ndani yake. Na watumwa wake
watamtumikia; nao watamwona uso wake, na jina lake litakuwa katika vipaji vya
nyuso zao. Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru
ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na
milele.
Kisha
akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu war oho za
manabii, alimtuma malaika wake kuwaonyesha watumwa wake mambo ambayo hayana
budi kuwako upesi. Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii
wa kitabu hiki.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
95:1 – 7 (K) 1Kor. 16:22, Ufu. 22:20
(K)
Maranatha, Uje, Bwana Yesu.
Njoni
tumwimbie Bwana,
Tumfanyie
shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje
mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie
shangwe kwa zaburi. (K)
Kwa
kuwa Bwana ni Mungu mkuu,
Na
mfalme mkuu juu ya miungu yote.
Mkononi
mwake zimo bonde za dunia.
Hata
vilele vya milima ni vyake.
Bahari
ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na
mikono yake iliiumba nchi kavu. (K)
Njoni,
tuabudu, tusujudu,
Tupige
magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa
maana ndiye Mungu wetu,
Na
sisi tu watu wa malisho yake,
Na
kondoo za mkono wake. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:135
Aleluya,
aleluya,
Umwangazie
mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:34-36
Yesu
aliwambia wanafunzi wake: Jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na
ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo;
kwa kuwa ndivyo itakavyowajilia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia nzima.
Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika hayo yote
yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment