MASOMO YA MISA, NOVEMBA 27, 2020
IJUMAA,
JUMA LA 34 LA MWAKA WA KANISA
SOMO
1
Ufu.
20:1 – 4, 11 – 21:2
Mimi,
Yohane, niliona malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa kuzimu, na
mnyororo mkubwa mkononi mwake. Akamshika yule joka, yule nyoka wa zamani,
ambaye ni Ibilisi na Shetani, akamfunga miaka elfu; akamtupa katika kuzimu,
akamfunga, akamtia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hata ile
miaka elfu itimie; na baada ya hayo yapasa afunguliwe muda mchache.
Kisha
nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, nao wakapewa hukumu; nami nikaona
roho zao waliokatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno
la Mungu, na hao wasiomsujudia yule mnyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea
ile chapa katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; nao wakawa hai,
wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu.
Kisha
nikaona kiti cha enzi, kikubwa, cheupe, nay eye aketiye juu yake; ambaye nchi
na mbingu zikakimbia uso wake, na mahali pao hapakuonekana. Nikawaona wafu,
wakubwa kwa wadogo, wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu
vikafunguliwa; na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima; na hao
wafu wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu, sawasawa
na matendo yao.
Bahari
ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu
waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake. Mauti
na Kuzimu zikatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndiyo mauti ya pili, yaani,
hilo ziwa la moto. Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha
uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.
Kisha
nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana za kwanza na nchi ya kwanza
zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu,
Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi
arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.
Neno
la Bwana… Tumshukuru Mungu.
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
84:2 – 5, 7 (K) Ufu. 21:3
(K)
Mungu anakuwa pamoja na watu.
Nafsi
yangu imeziona shauku nyua za Bwana,
Naam,
na kuzikondea.
Moyo
wangu na mwili wangu
Vinamlilia
Mungu aliye hai. (K)
Shomoro
naye ameona nyumba,
Na
mbayuwayu amejipatia kioto,
Alipoweka
makinda yake, kwenye madhabau zako,
Ee
Bwana wa majeshi,
Mfalme
wangu na Mungu wangu. (K)
Heri
wakaao nyumbani mwako,
Wanakuhimidi
daima.
Heri
ambaye nguvu zake zatoka kwako,
Na
njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake. (K)
SHANGILIO
Zab.
19:8
Aleluya,
aleluya,
Amri
ya Bwana ni safi, huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI
Lk.
21:29-33
Yesu
aliwaambia wanafunzi wake mfano, Utazameni mtini na miti mingine yote. Wakati
iishapo kuchipuka, mwaona na kutambua wenyewe ya kwamba majira ya mavuno
yamekwisha kuwa karibu. Nanyi kadhalika, mwonapo yamekwisha kuwa karibu. Nanyi
kadhalika, mwonapo mambo hayo yanaanza kutokea, tambueni ya kwamba ufalme wa
Mungu u karibu. Amin, nawaambieni, Kizazi hiki hakitapita hata hayo yote
yatimie. Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Neno
la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.
-------------------------
Copyright
© 2020, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment