“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumatatu,
Novemba 9, 2016,
Juma
la 32 la mwaka wa Kanisa
Sikukuu
ya Kutabarukiwa kwa Basilika la Laterani
Ez
47:1-2, 8-9, 12;
Zab
45:2-3, 5-6, 8-9;
1Kor
3: 9-11, 16-17;
Yn
2:13-22
HEKALU
LA MUNGU!
Katika
mwaka 592 Kabla ya kuja Kristo, Eziekeli alikutana na Mungu aliyemtumia kama
chombo, kwanza kuwaandaa watu wadhambi kwa maangamizi na baadae kutabiri juu ya
utengenezwaji upya wa hekalu. Baada ya muda mfupi 535 BC, ukaanza ujenzi wa
hekalu chini ya Zerubabeli aliyerudi kutoka utumwani Babeli na wayahudi zaidi
ya 42,000. Ujenzi ulikamilika 518 BC..
Hili
hekalu la pili lilijengwa katika hali ya kifahari chini ya Herodi mkuu ambaye
alitaka kumua Yesu, kama familia takatifu isingekimbilia Misri. Hili ni hekalu
ambalo Wayahudi walifanya sehemu ya kuuzia vitu na Yesu akawafukuza. Alitawanya
fedha zao na kupindua meza, akiwatoa ngombe na kondoo njee na alisema “…achene
kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa sehemu nyumba ya biashara”. Maneno haya ya
Yesu mara nyingi yaliwakasirisha viongozi. Lakini zaidi, jibu la Yesu juu ya
wao kutaka ishara ili kutoa ushuhuda wa anayo yafanya ulikuwa juu ya uwezo wao
wa kufikiri. Yesu alikuwa akiongelea kuhusu hekalu ambalo lilikuwa mwili wake
mwenyewe, ambao haujajengwa na mawe, lakini wao walikuwa wakiongelea kuhusu
hekalu lilojengwaa na Herodi.
Kwa
hili hekalu jipya la Agano jipya, Mt. Paulo anasema leo katika somo la pili
“hamkujua kwamba miili yenu ni hekalu la Mungu ambapo Roho wa Mungu anaishi
ndani yenu?” Mwili wa Kristo (Kanisa) lilizaliwa baada ya mwili wa Yesu kufa
pale kalvari na pazia la hekalu kupasuka kutoka juu mpaka chini (Mt 27: 50-51).
Yesu
anatuambia leo, sisi pia ni mahekalu ya Roho Mtakatifu, wa Mungu. Tukiwa
tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu, sisi ni mahekalu yalio barikiwa. Kama
viumbe wanao jitambua tunaweza na tunaalikwa kuitikia uwepo wa Mungu ndani
mwetu, kuwa hekalu binafsi na katika hali ya pekee. Leo tukiwa tunasherekea
kutabarukiwa kwa basilika la Laterani, mama wa makanisa yote ya Kikatoliki
ulimwenguni pote, tujenge tena upya hali ya umoja na mshikamano ambazo
zitatujenga na kututambulisha kila wakati kama wajumbe wa mwili wa Kristo.
Sala:
Bwana Yesu, kama ulivyo takasa hekalu, nitakase nami pia, nioshe, nifanye mpya,
nifanye nistahili kukupokea. Amina
-------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment