“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya Kila siku
Jumatano,
Novemba 4, 2020.
Juma
la 31 la Mwaka
Flp:
2:12-18;
Zab
27: 1.4.13-14,
Lk
14: 25-33.
GHARAMA
YA KUWA MFUASI!
Karibuni
ndugu zangu kwa tafakari ya neno la Mungu katika adhimisho la Misa Takatifu;
tafakari yetu ya leo inaanza kwa kuiangalia zaburi yetu ya wimbo wa katikati;
na hapa tunamkuta mzaburi akitangaza waziwazi kwamba Bwana ndiye ngome yake na
hakika hakuna cha kumtisha. Huu ni ushuhuda aliotoa Daudi kwani maishani mwake
aliionja huu ulinzi maalumu wa Bwana na leo anashuhudia mbele yetu kwamba Bwana
hakika ndiye alikuwa nguvu na ngome yake.
Ujumbe
huu wa Daudi unatilia mkazo pia ujumbe wa Paulo katika somo la kwanza. Paulo
anawasisitizia Wafilipi kujenga maisha yao katika Bwana. Wabakie watu wa imani
na utii hata kwa kile kipindi ambacho yeye hayupo kwao-wazidi kubakia kuwa
wema. Hii itawafanya wangae mbele ya watesi wao, mbele ya ulimwengu uliopotoka.
Ndilo
na sisi tunalokumbushwa na Paulo leo. Tumwambie Bwana kwamba wewe ni Mwamba
wetu. Hapa tutaweza kungaa ndani ya huu ulimwengu tukiwa nawe. Tukikosa hili
kwa hakika ndio tutakuwa tumekosa yote. Sehemu nyingi hatungai, tunakuwa watu
wa kuleta giza. Tunapokataa ukweli, kuwa watu wa kusingizia watu, kuiba vya
wengine, kuwatetea wenye navyo, na kukataa kuwasaidia majirani zetu hapa
tunatoa giza. Haya ni matendo yanayotufanya tushindwe kungaa.
Tufanye
matendo yatakayotufanya tungae tukiwa na Bwana.
Kwenye
injili yetu leo tunakutana na Yesu akisema kwamba kama hatuko tayari kubeba
msalaba kwa hakika hatutaweza kuwa wafuasi wake. Mfuasi wa Yesu lazima uoneshe
utayari wa kuvumilia. Hii ni tunu muhimu. Sio tunaogopa na kushindwa kuvumilia
hata kwa vitu vidogovidogo tu. Ni aibu kila siku kwa wakristo kushindwa na vitu
vidogo vidogo kwa kukosa uvumilivu. Wakristo wa mwanzo walionesha ukomavu kwa
kuwa hodari katika kuvumilia na wakafanikiwa sana.
Sisi
tusiwe watu wa kuogopa shida, tuvumilie misalaba ya familia zetu, masomo,
rafiki na majirani. Kwa uvumilivu wetu, tutayaokoa maisha yetu. Wengi
tutapoteza mengi kwa sababu ya kukosa uvumilivu. Tumuombe Mungu atusaidie.
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment