“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Ijumaa,
Octoba 30, 2020,
Juma
la 30 la Mwaka
Fili
1: 1-11;
Zab 110:
1-6
Lk
14: 1-6.
KUWA
NA HURUMA
Leo
Yesu anwauliza Mafarisayo swali “je, ni kinyume cha sheria kumponya mtu siku ya
Sabato?” Mafarisayo hawana jibu. Baada ya kumponya mtu aliyekuwa na ukoma,
anawaonya Mafarisayo kwa kushindwa kuonesha huruma, na badala yake kutumia
sababu za kisheria.
Mafarisayo
hawakuwa na huruma kwa ndugu zao, huyu mtu mwenye ukoma, walikuwa
wakijishughulisha na Sabato. Yesu anawauliza kwa mfano alikuwa mwana wao au
alikuwa ni punda wao? Yesu anaonesha mioyo baridi ya Mafarisayo, ambao walifikiria
kwamba punda ni zaidi ya wana wa Mungu waliokuwa wagonjwa na maskini.
Kama
tukijaribu kumwangalia huyu mtu alieponywa. Ugonjwa ambao ulikuwa ukimtesa
ulikuwa ni ukoma, ambapo mwili hutoa maji maji. Sisi kama Mafarisayo huenda
tukawa tunaugua ugonjwa kama wa Mafarisayo-pengine si katika hali ya mwili.
Hili linakuja pale ambao tunajaza mioyo yetu na ubinafsi na kushindwa kupenda
kizuri kwa ajili ya wengine. Ni Yesu mwenyewe anayeweza kuondoa ukame wetu na
ubinafsi wetu wa kushindwa kuwapenda wengine kwa uhuru.
Cha
muhimu ni kuona mwitikio wetu juu ya wale wanao hitaji msaada wetu, huwa tuna
visingizio vingi vya kutoa. Kwa mfano swala la wakimbizi, Baba mtakatifu
Fransisko la kuwasahauri parokia na wakristo kuwakaribisha wakimbizi
halikupokelewa sana. Swala hili wamelichukulia katika mijadala. Lakini mbaya
zaidi hakuna hata tendo lolote la huruma wanalopendekeza wale wanao pinga.
Leo,
tujiulize sisi wenyewe kama nasi tuna mioyo baridi. Je, tupo tayari kuvuka
mipaka ya akili zetu na mipaka ya roho zetu kwa aili ya kuwa wakarimu?
Sala:
Bwana Yesu njoo katika moyo wangu, katika hali yangu ya maisha. Njoo zama,
katika kazi, kati ya marafiki, katika magumu yangu, wakati wa matatizo, na
katika vitu vyangu. Nisaidie mimi niweze kuwa mkarimu kwa ndugu zangu. Yesu,
nakuamini wewe. Amina
------------------------
Copyright
©2013-2020 ©FurKat, FurahayaKikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment