MASOMO
YA MISA,
JUMAPILI,
SEPTEMBA 6, 2026
JUMA
LA 23 LA MWAKA
________
MWANZO
Zab.
119:137, 124
Ee
Bwana, wewe ndiwe mwenye haki, na hukumu zako ni za adili. Kama zilivyo rehema
zako umtendee mtumishi wako.
________
SOMO
I
Eze.
33:7-9
Basi
wewe, mwanadamu, nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israeli; basi ulisikie
neno hili kinywani mwangu, ukawape maonyo yangu. Nimwambiapo mtu mbaya, Ewe mtu
mbaya, hakika utakufa, nawe husemi neno la kumwonya mtu huyo, aiache njia yake,
mtu mbaya huyo atakufa katika uovu wake, lakini damu yake nitaitaka mkononi
mwako. Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache;
wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho
yako.
Neno
la Bwana...Tumshukuru Mungu
________
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
95:1-2, 6-9 (K) 7-8
(K)
Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake!
Tusifanye
migumu mioyo yetu.
Njoni
tumwimbie Bwana,
Tumfanyie
shangwe mwamba wa wokovu wetu.
Tuje
mbele yake kwa shukrani,
Tumfanyie
shangwe kwa zaburi. (K)
Njoni,
tuabudu, tusujudu,
Tupige
magoti mbele za Bwana aliyetuumba.
Kwa
maana ndiye Mungu wetu,
Na
sisi tu watu wa malisho yake,
Na
kondoo za mkono wake. (K)
Ingekuwa
heri leo msikie sauti yake!
Msifanye
migumu mioyo yenu;
Kama
vile huko Meriba;
Kama
siku ile ya Masa jangwani,
Hapo
waliponijaribu baba zetu;
Wakanipima,
wakayaona matendo yangu. (K)
________
SOMO
2
Rum.
13:8-10
Msiwiwe
na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza
sharia. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani, na ikiwapo amri
nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako
kama nafsi yako. Pendo halimfanyii jirani neno baya, basi pendo ndilo utimilifu
wa sheria.
Neno
la Bwana...Tumshukuru Mungu
________
SHANGILIO
Yn.
14:23
Aleluya,
aleluya,
Mtu
akinipenda, atalishika neno langu;
Na
baba yangu atampenda; Nasi tutakuja kwake.
Aleluya.
________
INJILI
Mt.
18:15-20
Siku
ile Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe
na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo. La, kama hasikii, chukua
pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au
watatu kila neno lithibitike. Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na
asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni;
na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Tena
nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote
watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa walipo
wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
________
-------------------------
Copyright
© 2026, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see
www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment