“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Alhamisi,
Septemba 17, 2026,
Juma
la 24 la Mwaka
1Kor
15:1-11
Zab
117: 1-2, 15-17, 28;
Lk7:
36-50.
KUOMBA
HURUMA
Karibuni
sana ndugu zangu wapendwa kwa adhimisho la Misa Takatifu tena asubuhi ya leo.
Bado tunaendelea kuongozwa na tafakari ya neno la Mungu toka katika kitabu cha
waraka wa kwanza wa mtume Paulo kwa Wakorintho. Na bado anaendelea kujibu
maswali na changamoto zilizoikumba ile jumuiya. Na leo anazungumzia changamoto
juu ya suala la ufufuko. Wakristo wa Korintho waliishi kati ya wanafalsafa
waliowakejeli juu ya suala la ufufuko baada ya wafu. Walikuwako wanafalsafa
kama akina Epicureans waliosisitizia juu ya kuponda mali na anasa. Wakati huu
falsafa hii ilikuwa imeshika kasi sana na hawakuamini ufufuko.
Wakristo
walimtegemea Kristo aje kwa haraka ili basi awafufue wale wakristo waliokuwa
wakifariki kabla ya Kristo kuja ili basi wale wanafalsafa wapate kuoneshwa
kwamba walichokifundisha sio sahihi. Lakini basi Yesu hakufika kwa haraka vile
walivyokuwa wakihisi na hivyo basi wakauliza je, kwa nini? Wanafalsafa hawa
waliwakejeli sana wakristo na imani yao juu ya ufufuko kwa kuwaambia kwamba ni
uzushi.
Lakini
basi Paulo anajibu suala hili na kwa kuanza kusema kwamba kwanza suala la
ufufuko ni la kweli kabisa na si la uzushi kama wanafalsafa hawa wanavyodai.
Anaanza hoja yake kwa kumtaja Yesu-yeye alishuhudiwa na watu tena kati yetu
akifa msalabani kabisa, akafa na akazikwa-lakini pia alishuhudiwa na baadhi
yetu akiwa amefufuka tena ikiwapo mimi-sasa anawauliza-ninyi mnasemaje kuhusu
hili? Ni uzushi tena? Anawaambia jamani bakini katika imani yenu-msidanganywe
na hawa watu; mtumaini Kristo.
Ndivyo
inavyotokea na kwetu ndugu zangu. Bado tunadanganywa na falsafa mbalimbali na
kuziungamia. Tumedanganywa na mitandao mbalimbali na kupotezea muda huko kana
kwamba kila kitu kisemwacho nayo ni sahihi. Tunajisikia hofu kubwa pale
tunaposafiri bila simu kuliko pale tusafiripo bila hata rozari mfukoni.
Tunakuwa tayari kuacha rozari au hata biblia kuliko simu-lengo ni kwamba simu
itatulinda, itatuburudisha kwa kutupatia habari mbalimbali za kwenye mitandao.
Tuna hofu yakukosa habari kuliko kukosa kanisani.
Kwenye
somo la kwanza tunakutana na Yesu akimpinga mfarisayo aliyepinga yeye kupakwa
mafuta na mama mmoja. Haya ni matendo aliyoyashindwa yule mfarisayo lakini
akayaweza yule mama. Yule mama alionesha heshima kwa Yesu kuliko huyu
mfarisayo. Mfarisayo aliona wivu kana kwamba yule mama alikuwa akijipatia sifa
zaidi kuliko yeye. Hata majibu yake anayomueleza Yesu chanzo chake ni wivu.
Anataka Yesu asitendewe uzuri kwa sababu ya wivu wake. Hata na sisi tupo
hivihivi ndugu zangu. Wengi wetu tuna wivu; hatutaki wengine watendewe wema na
sisi hatuko tayari kuwatendea. Tukiona wengine wakiutenda tunakasirika, ati
tunataka wasifaidi? Tukiona wengine wakitendewa wema yabidi tufurahi zaidi.
Kama huwezi kuutenda wema, mwingine ataweza.
------------------------
Copyright
©2013-2026 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com.
No comments:
Post a Comment