“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Afakari
ya kila siku
Ijumaa,
Septemba 12, 2025.
Juma
la 23 la Mwaka wa Kanisa
1
Tim 1:1-2, 12-14;
Zab
16:1-2,5,7-8, 11;
Lk
6: 39-42
HESHIMA NA MAJITOLEO
Tumeumbwa
kushirikiana kama watu walio sawa na si kwa namna ya matabaka. Tunatakiwa
kutambua vipawa vyetu na kushirikishana. Mt. Paulo anasema katika waraka wake
wa kwanza kwa Timotheo kuwa, anakiri kuwa alitambua wito wake katika ujinga
wake na katika kutokuamini kwake. Tuombe Neema hii aliyopokea Mt. Paulo ili
nasi tubadilishwe katika maisha yetu.
Tunaalikwa
kujifunza kutoka kwa wenzetu. Kila amtu anamtegemea mwenzake katika ufahamu na
nguvu zinazotofautiana. Tunahitaji hekima na busara za majirani zetu. Papa
Francis anasisitiza juu ya undugu katika kanisa zima kwa ujumla.
Kwa sababu
hatujakamilika katika kung’amua mambo ya watu wanaotuzunguka, inakuwa rahisi
sana kuhukumu wengine. Tunaweza kusema kuwa sote tunaweza kuona lakini
kiuhalisia baadhi yetu ni vipofu. Bwana wetu Yesu Kristo anatuonesha kuwa sisi
ni vipofu kwa namna Fulani, na mara nyingi kipofu anamuongoza kipofu. Mara
chache sana mtu aonaye kumuongoza yule aliye kipofu.
Yesu
anatubadilishia mfano ili tuweze kumuelewa Zaidi. Yesu anatupa mfano wa mtu
anayetazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yake, na boriti iliyo ndani
yake mwenyewe haiangalii.Yesu anaposema kutoa boriti kwanzaa kwenye jicho lako
mwenyewe maana yake kutambua madhaifu yetu kabla ya kuona madhaifu ya wengine.
Mara nyingi tunashindwa kutambua kinachoendelea katika maisha ya wenzetu hivyo
tunaishia kuwahukumu tu. Mungu anayeona undani kila moyo, ni mwenye huruma kwa
wote hata kwa wale wasiostahili. Leo tunaalikwa kuwa na huruma na msamaha kwa
wengine.
No comments:
Post a Comment