
“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumapili
Agosti, 17, 2025
Juma
la 20 la Mwaka C wa Kanisa
Yer:
38:4-6.8-10
Ebr.12:1-4
Lk
12: 49-53
MUNGU
NI MOTO UNAOPENDEZESHA VYOTE
Katika
soma la kwanza tumeona nabii Yeremia alitumwa na Mungu kuwaeleza wayahudi kwamba
mji Yerusalemu utatekwa na jeshi la mfalme wa Bebeli. Lakini wakuu wa Yuda
walichukizwa na ukweli huo wakaamua Yeremia auawe. Kutupwa Yeremia katika matope
na kuokolewa kwake kunatazamwa na wakristo kama mfano wa kifo na ufufuko wa
Yesu.
katika Soma
la pili mtume Paulo anatuamibia waraka huu uantusimulia namna watakatifu
walivyovumilia taabu na kupata tuzo lao; pia namna Yesu alivyostahimili mateso
na kupata utukufu. Uvumilivu wa watakatifu hao na hasa wa Bwana Yesu ni mfano
wa hizimo katikakuzichukua taabu zetu za kila siku tukitaka kuufikia utukufu
huo.
Katika
Somo la Injili Yesu anatupa tahadhari nyingine kwamba kwa ujio wake yaweza kuwa
amekuja kuwasha moto duniani. Na hili kweli linatokea nyakati zetu,
tumeshuhudia familia zikitengana kwa kigezo cha Injili tena wote wakiwa wafuasi
wa Kristo. Wengine hujidai wanamuelewa Kristo zaidi na kuwadharau wengine.
Wengine huamka hata usiku wa manane na kuwasumbua wengine kwa sala za kelele
kwa kisingizio wanafukuza pepo na kuwafanya wengine wasilale. Wengine hujifanya
wafafanuzi wazuri wa maandiko zaidi kuliko wengine na hivyo kuishia kushindana.
Yesu haya aliyatambua yatakuwepo. Paulo anatupatia jibu zuri sana katika (Ef
3:14-21), hamna namna nyingine ya kuonesha kwamba sisi ni wafuasi wa Kristo
isipokuwa kwa njia ya upendo. Utengano sio sifa ya Kristo.
Yesu
aliwashtuwa wafuasi wake pale aliposema kuwa amekuja kutupa moto na kusababisha
mgawanyiko badala ya amani duniani. Je, ni aina gani ya moto ambao Yesu
alikuwanao akilini mwake? Moto katika neno la Kibiblia ulihusianishwa na Mungu
pamoja na kuhusianishwa na matendo yake ulimwenguni katika maisha ya watu wake.
Wakati
mwingine Mungu anadhihirisha uwepo wake kwa uwepo wa moto, kama vile kichaka
kiwakacho ambacho hakiteketei alipoongea na Musa (Kut 3:2). Alama ya moto
ilitumika pia kuwakilisha utukufu wa Mungu (Eze 1:4, 13), uwepo wa ulinzi wake
(2Fal 6:17), utakatifu wake (Kum 4:24), hukumu ya haki (Zek 13:9), na hasira
yake dhidi ya dhambi (Isa 66:15-16). Pia imetumika pia ikimaanisha Roho
Mtakatifu (Mt 3:11 na Mat 2:3). Moto wa Mungu unasafisha na huondoa uchafu, na
unavuvia mwanga na hofu ya kumuabudu Mungu na nguvu ya neno lake ndani yetu.
Basi
tuchukue mfano mmoja kutoka kwenye Biblia uhusuo moto – kichaka kiwakacho
katika kitabu cha Kutoka. Kichaka chaonekana kuwa kinawaka tu badala ya
kuteketea. Sifa ya asili ya moto ni kuchoma na kuteketeza. Lakini kinachotokea
hapa ni hali ya tofauti. Je, unasema nini juu ya Mungu wetu? Ndio Mungu wetu ni
moto, sio moto uharibuo bali moto unaobadilisha. Unatuunguza sisi kufikia
uzuri. Mara utakapo unguzwa na moto huu katika uhalisia unakuwa kiumbe kipya,
unatoka kwenye uovu na kusimama njee. Kama upo katika familia yako ya watu
wanne na ukawa umeunguzwa mpaka kufikia uzuri katika uhalisia utakuwa nje.
Unasimama njee ukiwa tofauti na hapo huenda ukachukiwa au kupendwa au kuigwa.
Inawezekana familiya yetu na marafiki zetu kuwa maadui zetu. Kama mawazo yao
yatatuzuia sisi kutenda yale tunayoyajua kuwa Mungu anapenda sisi kuyafanya ni
dhahiri tutamtii Mungu zaidi kuliko wao, na hapo huenda uadui ukawepo. Je,
upendo wa Yesu Kristo unakusukuma wewe kumuweka Mungu kwanza kwa yale yote
uyatendayo (2 Kor 5:14)?
Tusitumie
pia sala kama kisingizio cha kuwakashifu wale wasio sali. Tusijione wema zaidi
kwasababu tu sisi tunaenda kanisani na wengine hawaendi. Badala yake sisi
tuwaombee waregevu na kuwashauri kwa upendo na upole ili waweze kuvutwa nao
kumtumikia Kristo. Tusiwashe moto duniani wa fujo kwakutumia Injili ya Kristo.
Sala:
Bwana, naomba upendo wako unitawale na uyarekebishe maisha yangu. Amina
No comments:
Post a Comment