MASOMO
YA MISA,
JUMATATU,
AGOSTI 4, 2025
JUMA
LA 18 LA MWAKA
SOMO
1
Hes.
11 :4-15
Wana
wa Israeli walilia wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? Twakumbuka samaki
tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu,
na vitunguu saumu; lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote;
hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hi; mana tu.
Na
hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtarna, na kuonekana kwake kulikuwa kama
kuonekana kwake bedola. Watu wakazunguka-zunguka na kuikusanya, kisha wakaisaga
kwa mawe ya kusagia, au kuitwanga katika vinu, kisha wakaitokosa nyunguni, na
kuandaa mikate; na tamaa yake ilikuwa kama tamu ya mafuta mapya. Umande
ulipoyaangukia marago wakati wa usiku, hiyo mana ilianguka pamoja nao.
Basi
Musa akawasikia watu wakilia katika jamaa zao zote, kila mtu mlangoni pa hema
yake; na hasira za Bwana zikawaka sana; Musa naye akakasirika.
Musa
akamwambia Bwana, Mbona umenitenda uovu mimi mtumishi wako? kwa nini sikupata
neema machoni pako, hata ukanitwika mzigo wa watu hawa wote juu yangu? Je! ni
mimi niliyewatungisha mimba watu hawa wote? je! ni mimi nilivewazaa, hata ikawa
wewe kuniambia, Haya, wachukue kifuani mwako, mfano wa baba mwenye kulea
achukuavyo mtoto aamwaye, wende nao mpaka nchi uliyowaapia baba zao? Nipate
wapi nyama ya kuwapa watu hawa wote? kwani wanililia, wakisema, Tupe nyama,
tupate kula. Mimi siwezi kuwachukua watu hawa wote peke yangu, kwa kuwa ni
mzigo mzito sana wa kunishinda. Na kama ukinitenda hivi, nakuomba uniulie
mbali, kwamba nimepata fadhili mbele ya macho yako; nami nisiyaone haya mashaka
yangu.
Neno
la Mungu...Tumshukuru Mungu
WIMBO
WA KATIKATI
Zab.
81 :11-16 (K) 1
(K)
Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha.
Watu
wangu hawakuisikiliza sauti yangu,
Wala
Israeli hawakunitaka.
Nikawaacha
wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao,
Waenende
katika mashauri yao. (K)
Laiti
watu wangu wangenisikiliza,
Na
Israeli angeenenda katika njia zangu;
Ningewadhili
adui zao kwa upesi,
Na
juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu. (K)
Wamchukiao
Bwana wangenyenyekea mbele zake,
Bali
wakati wao ungedumu milele.
Naam,
ningewalisha kwa unono wa ngano,
Ningewashibisha
kwa asali itokayo mwambani. (K)
SHANGILIO
Zab.
119:34
Aleluya,
aleluya,
Unifahamishe
nami nitaishika sheria yako, nitaitii kwa moyo wangu wote.
Aleluya.
INJILI
Mt.
14: 13-21
Yesu
aliposikia habari ya kuuawa kwa Yohane Mbatizaji, aliondoka huko katika chombo,
akaenda mahali pasipo watu, faraghani. Na makutano waliposikia, walimfuata kwa
miguu kutoka miiini mwao. Yesu akatoka, akaona mkutano mkuu. akawahurumia,
akawaponya wagonjwa wao.
Hata
kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika
tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini,
wakajinunulie vyakula. Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi
kula. Wakamwambia, Hatuna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili.
Akasema, Nileteeni hapa.
Akawaagiza
makutano wakati katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki
wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa
wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano. Wakala wote wakashiba; wakayaokota
masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa. Nao waliokula
walikuwa wanaume wapata elfu tano, bila wanawake na watoto.
Neno
la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
Copyright
© 2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora
– Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment