ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Tafakari
ya kila siku
Jumanne,
Agosti 19, 2025
Juma
la 20 la Mwaka wa Kanisa
Amu:
6:11-24
Zab:
85:8-13
Mt
19:23- 30
KUACHA
YOTE NA KUMFUATA KRISTO!
Kilele
cha mwisho kabisa cha mwanadamu ni kujua, kupenda, kumtumikia Mungu na
kufurahia maisha ya milele pamoja naye daima. Na Mungu anapenda kutushirikisha
uzima huu wa milele. Ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hatuwezi kupata uzima huu kwa
nguvu za kibinadamu. Tungeachiwa sisi tu, ingekuwa vigumu sana kwetu sisi
kuupata. Lakini kwa neema ya Mungu yote yanawezekana. Lakini, mali na utajiri
vinaonekana viashiria vinavyo hatarisha kutokuupata ufalme huu wa milele.
Katika ulimwengu huu wa sasa wenye mambo mengi inakuwa vigumu kwa wengine
kukwepa hili. Ni jambo kubwa la kweli “kuacha yote” lakini kubwa zaidi
“kumfuata Yesu”.
Kumfuata
Yesu ni kazi yetu. Katika hili linabeba ukombozi wa mwanadamu, lakini hatuwezi
kumfuata Kristo kama hatutaacha yote yanayotufunga tushindwe kumfuata. Nabii
Ezekiel katika somo la kwanza anatoa angalisho kwa mji wa Tiro na viongozi wake
waliopata mafanikio makubwa na nguvu. Wameweka ulinzi wao na Imani yao katika
utajiri na mali ambavyo vimegeuka kuwa miungu yao.
Lakini
Petro anasema, “tumeacha yote” sio tuu vitu vya ulimwengu, lakini pia tamaa
zinazopendwa na mioyo yetu. Wanaobaki wakiwa wameshikilia baadhi ya vitu
inakuwa hawajaacha yote. Kwanini anatoa ujumbe mkali namna hiyo kwa matajiri?
Kwanini Yesu anaongea sana kuhusu mali? Ni kwasababu mali inaweza kutufanya
tusiwe huru au kutupa uhuru wa ouongo. Wengine wameshindwa kumfuata Yesu
kwasababu ina maana ya kuacha baadhi ya uhusiano, na wengine kama yule tajiri,
ni kwasababu watapoteza nafasi yao ya heshima au njia zao za kupata mali. Wewe
je?
Sala:
Bwana, naomba nikufanye wewe wa kwanza katika maisha yangu na nikuchague wewe
kwa uhuru kamili hata kama kukufuata inagarimu.
Copyright
©2013-2025 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment