"ASALI ITOKAYO MWAMBANI"
Tafakari ya kila siku
Jumapili, Julai 10, 2022.
Juma la 15 la Mwaka
Deut. 30:10-14
Col 1:15-20
Lk 10:25-37
"Msamaria Mwema".
Leo tuna hadithi moja maarufu ya injili, "Msamaria Mwema". Kuna watu wanne katika hadithi hii:
1. Kuhani wa Kiyahudi, mtu wa kidini ambaye anayehudumia hekaluni,
2. Mlawi, ambaye pia ni mtu wa kidini,
3. Msamaria msafiri, aliyeonekana na Wayahudi kuwa mgeni, na mtu ambaye hutakiwi kuwa na mahusiano naye.
4. Mtu asiyejulikana, aliyeanguka mikononi mwa wanyg’ani, aliyejeruhiwa, labda myahudi.
Leo Yesu anatuambia hadithi ambayo inasimama kama katikati ya sheria za utakaso za Kiyahudi na upendo wa ukarimu wa kibinadamu. Pia inasimama kama mfano kinyume wa utamaduni wetu wa ulimwengu wa sasa ya 'kutupa' kama anayefaidika ni siyo wewe au siyo kwa manufaa ya kibinafsi.
Kuhani na Mlewi huenda walikuwa njiani kwenda Hekaluni. Hawakuweza kujihusisha na mtu aliyejeruhiwa. Kugusa mtu huyu ambaye damu yake ilikuwa inamwagika, na kugusa damu ingewafanya wanajisi, kuingia hekaluni na kummwabudu Mungu. Lakini Msamaria aliyekuwa anapita njia kwa biashara fulani, anaacha kazi zake na anamhudumia mtu aliyejeruhiwa.
Hata leo tunaweza kujilinganisha na mmojawapo wa hawa watu watatu. Leo tunaona watu badala ya kumsaidia mtu aliyejeruhiwa, wanajihusisha na kupiga sefie, video za kwa ajili ya kuweka kwenye vyombo vya kijamii (social media). Tunatafuta haki kwa kusema huenda mwingine ameshaiita ambulens. Jiulize ni mara ngapi umeacha kusaidia mtu mwingine akiwa katika shida: inawezekana mtu aliyepata ajali, mtu aliyepata shida ya kuharibika kwa gari, ombaomba na mhitaji anayehitaji nguo na matibabu. Matukio haya ni ya kwaida, wakati mwingine tunaonyesha hisia zetu kwa haya. Lakini mbele ya kipaumbele chetu cha kazi, familia, dini, tunayasahau wahitaji hawa.
Wakati Mama Teresa alianza nyumba huko Kolkota kwa wanaokufa, mbele ya Hekalu la mungu Kali, wengi walimpinga kwamba anafanya hiyo kwa kuwabadilisha Wahindu na Waislam kuwa wakristo. Lakini wakati Kamishna wa Polisi aliyepokea malalamiko ya watu aliwaambia: "Nitamfukuza mwanamke huyu kutoka hapa, nitamfunga gerezani (wote walianza kupiga makofi)" na akasema "Nitafanya hivyo ikiwa mtawachukua wote hawa wanaokufa, wagonjwa nyumbani zenu na kuwatunza kama mwanamke huyu.”Kwa watu kama Mama Teresa, mwenyeheri Damien wa Molokoi, upendo ulikuwa kitu cha kipaumbele. Ilikuwa kwa njia ya upendo, upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani, waliufikia umoja na Mungu.
Hadithi hii ni jibu kwa swali: "nani ni jirani yangu?" Yeye sio tu jirani, wala mwananchi mwenzangu, wala Mkatoliki mwenzangu lakini mtu anayemsaidia ndugu aliyekuwa na mahitaji au shida Fulani. Anayesaidia ndugu yake katika shida ni jirani halisi katika injili.
"Mpende jirani yako kama wewe mwenyewe" ni mkono mmoja wa amri kuu. "Ni nani jirani yangu?" Ni swali muhimu katika kutekeleza amri. Kila mmoja ana uaminifu kuuliza swali hili. Njia nyingine ya kuuliza ni, "Ni nani katika maisha yangu nina nia ya kusaidia?" Ni vigezo gani ya kumsaidia mtu mwingine? Je! Familia, marafiki, rangi, dini, maadili, huingia kwenye picha? Vipi kuhusu mtu anayenichukia? mlevi? kahaba? Mhalifu? Kwa kujibu kwa uaminifu swali, "Ni nani jirani yangu?", Ninajifunza mengi juu ya aina ya mtu niliyo mimi, na aina gani ya jirani ni mimi.
Swala: Bwana! Nisaidie kuwa jirani mwema. Amina
Copyright ©2013-2022 ©FurKat, Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment