MASOMO YA MISA, JUMANNE, JULAI 1,
2025
JUMA LA 13 LA
MWAKA
SOMO 1
Mwa. 19 :15-29
Hata alfajiri
ndipo malaika walimhimiza Lutu, wakisema, Ondoka, mtwae mkeo na binti zako
wawili waliopo hapa, usipotee katika maovu ya mji huu. Akakawia-kawia; nao wale
watu wakamshika mkono, na mkono wa mkewe, mkono wa binti zake wawili, kwa jinsi Bwana alivyohurumia,
wakamtoa wakamweka nje ya mji.
Ikawa walipomtoa
nje, mmoja alisema, Jiponye nafsi yako; usitazame nyuma, wala usisimame katika
hilo bonde po pote; ujiponye mlimani, usije ukapotea. Lutu akawaambia, Sivyo,
bwana wangu! tazama, mtumwa wako ameona kibali machoni pako, nawe umezidisha
rehema zako ulizonifanyia kwa kuponya nafsi yangu, nami siwezi kukimbilia
mlimani nisipatwe na yale mabaya, nikafa. Basi mji huu u karibu, niukimbilie,
nao ni mdogo, nijiponye sasa huko, sio mdogo huu? Na nafsi yangu itaishi.
Akamwambia, Tazama, nimekukubali hata kwa neno hili, kwamba sitauangamiza mji
huo uliounena. Hima, ujiponye huko, maana siwezi kufanya neno lo lote, hata
uingiapo humo. Kwa hiyo jina la mji ule likaitwa Soari.
Jua lilikuwa
limechomoza juu ya nchi Lutu alipoingia Soari. Ndipo Bwana akanyesha juu ya
Sodoma na juu ya Gomora kiberiti na moto toka mbinguni kwa Bwana. Akaangusha
miji hiyo na Bonde lote, na wote waiiokaa katika miji hiyo, na yote yaliyomea
katika nchi ile. Lakini mkewe Lutu akatazama nyuma yake, akawa nguzo ya chumvi.
Ibrahimu akatoka
asubuhi kwenda mahali aliposimama mbele za Bwana, nave akatazama upande wa
Sodoma na Gomora na nchi yote ya hilo Bonde, akaona, na tazama, moshi wa nchi
ukapanda, kama moshi wa tanuru. Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu
akamkumbuka Ibrahimu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo
aliyokaa Lutu.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA
KATIKATI
Zab. 26:2-3,9-12
(K) 3
(K) Fadhili
zako, ee Bwana, zi mbele ya macho yangu.
Ee Bwana,
unijaribu na kunipima;
Unisafishe mtima
wangu na moyo wangu.
Maana fadhili
zako zi mbele ya macho yangu,
Nami nimekwenda
katika kweli yako. (K)
Usiiondoe nafsi
yangu pamoja na wakosaji,
Wala uhai wangu
pamoja na watu wa damu.
Mikononi mwao
mna madhara,
Na mkono wao wa
kuume umejaa rushwa. (K)
Ila mimi
nitakwenda kwa ukamilifu wangu;
Unikomboe,
unifanyie fadhili.
Mguu wangu
umesimama palipo sawa;
Katika
makusanyiko nifamhimidi Bwana. (K)
SHANGILIO
Yn. 14:23
Aleluya,
aleluya,
Mtu akinipenda,
atalishika neno langu,
na Baba yangu
atampenda,
na sisi tutakuja
kwake.
Aleluya.
INJILI
Mt. 8:23-27
Yesu alipanda
chomboni, wanafunzi wake wakamfuata. Kukawa msukosuko mkuu baharini, hata
chombo kikafunikizwa na mawimbi; naye alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake
wakamwendea, wakamwamsha, wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia. Akawaambia,
Mbona mmekuwa waoga, enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na
bahari; kukawa shwari kuu. Wale watu wakamka wakisema, Huyu ni mtu wa namna
gani hata pepo na bahari zamtii?
Injili ya
Bwana........Sifa kwako Ee Kristo
Copyright ©
2025, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment