MASOMO YA MISA,
JULAI 27, 2025
DOMINIKA YA 17 YA
MWAKA
SOMO 1
Mwa. 18 :20-32
Bwana alisema, Kwa
kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi. na dhambi zao zimeongezeka sana.
basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na
kama sivyo, nitajua. Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini
Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia, akasema,
Je! utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini
katika mji, utaharibu, wala hu- tauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki
waliomo? Hasha, usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye
haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Bwana
akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote
kwa ajili yao. Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami
ni mavumbi na majivu tu. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye
haki, Je! utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona
humo arobaini na watano. Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana
humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema, Bwana
asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema,
Sitafanya, nikiona humo thelathini. Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana,
huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema. Sitaharibu kwa ajili ya hao
ishirini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu. Huenda
wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.
Neno la Mungu...
Tumshukuru Mungu
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 138:1-3,6-9
(K)3
(K) Siku ile
niliyokuita uliniitikia, Ukanifariji nafsi kwa kunitia nguvu.
Nitakushukuru kwa
moyo wangu wote,
Mbele ya miungu
nitakuimbia zaburi.
Nitasujudu
nikilikabili hekalu lako takatifu, (K)
Nitalishukuru jina
lako,
Kwa ajili ya
fadhili zako na uaminifu wako,
Kwa maana umekuza
ahadi yako,
Kuliko jina lako
lote.
Siku ile
niliyokuita uliniitikiu,
Ukanifariji nafsi
kwa kunitia nguvu. (K)
Ingawa Bwana yuko
juu, amwona mnyenyekevu,
Naye amjua mwenyc
kujivuna tokca mbali.
Nijapokwenda kati
ya shida utanihuisha,
Utanyosha mkono juu
ya hasira ya adui zangu. (K)
Na mkono wako wa
kuume utaniokoa.
Bwana atanitimiliza
mambo yangu;
Ec Bwana, fadhili
zako ni za milele;
Usiziache kazi za
mikono yako. (K)
SOMO 2
Kol 2 : 12-14
Mkazikwa pamoja na
Kristo katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini
nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu
ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye,
akiisha kutusamehe makosa yotc; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena,
akaigongomea msalabani.
Neno la Mungu...
Tumshukuru Mungu
SHANGILIO
Yn. 14 :23
Aleluya, aleluya,
Mtu akinipenda,
atashika neno langu, na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake.
Aleluya.
INJILI
Lk. 11:1-13
Yesu alipokuwa
mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia,
Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi
wake. Akawaambia, Msalipo, semeni, Baba [yetu uliye mbinguni]. Jina lako
litakaswe, Ufalme wako uje, [Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko
mbinguni.] Utupe siku kwa siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa
sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie maiaribuni [lakini tuokoe na
vule mwovu].
Akawaambia, Ni nani
kwenu aliye na rafiki, akamwendea usiku wa manane, na kumwambia, Rafifi yangu,
nikopeshe mikate mitatu, kwa sababu rafiki yangu amefika kwangu, atoka
safarini, nami sina kitu cha kuweka mbele yake; na yule wa ndani amjibu
akisema, Usinitaabishe; mlango umekwisha fungwa. nasi tumelala kitandani mimi
na watoto wangu; siwezi kuondoka nikupe? Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa
haondoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba,
ataondoka na kumpa kadiri ya haja yake.
Nami nawaambia,
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Kwa
kuwa kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Maana ni yupi kwenu aliye baba, ambaye mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? au
samaki, badala ya samaki atampa nyoka? au akimwomba yai, atampa nge? Basi,
ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Baba aliye
mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao wamwombao?
Neno la Bwana...
Sifa kwako, ee Kristo
Copyright © 2025, "MASOMO YA
MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings
reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment