“MBEGU ZA UZIMA”
Tafakari ya Dominika
Jumapili, Juni 12, 2022.
Sherehe ya Utatu
Mtakatifu
Mit: 8:22-31
Roma: 5:1-5
Yn: 16:12-16
MUNGU KATIKA UTATU
Wakatoliki , duniani
kote, sio kwamba wanaamini Mungu tu, bali wanaamini Mungu mmoja. Lakini Mungu
wetu yupo katika Utatu- Utatu katika umoja na umoja katika Utatu. Kila mmoja ni
Mungu kwa asili na wote ni Mungu mmoja. Sawa katika Nguvu, ni wa milele na wana
utukufu. Fumbo hili kuu linaweza kuchukuliwa kama fumbo lililo kuu kabisa
katika Biblia Takatifu. Wakristo tunaamini fumbo hili kuu ndani ya mamlaka ya
Yesu Kristo na Agano Jipya. Ni moja wapo ya fumbo kubwa la ndani kabisa
lililofunuliwa na lililopo juu kabisa kupita akili ya mwanadamu. Yesu mara
nyingi ameongea kuhusu Mungu kama Baba yake. Sauti ya Baba ilisikika wakati wa
ubatizo wa Yesu; “Huyu ni mwanangu mpendwa niliye pendezwa naye msikilizeni
yeye”. Yesu alipo ngara sura, pia, sauti hiyo hiyo ilisikika ikisema maneno
hayo hayo. Katika matukio yote uwepo wa wingu jeupe ilionyesha uwepo wa Roho
Mtakatifu, ambaye Yesu aliwaahidia wakati alipokuwa akipaa kwenda kwa Baba,
“nitawapa msaidizi Mwingine-Roho wa kweli anayetoka kwa Baba”.
Yesu anatuambia kwamba,
Mungu aliupenda sana ulimwengu mpaka akamtuma mwanaye ulimwenguni, ili wote
watakao muamini wasipotee bali wawe na uzima wa milele (Yn 3:16). Anaelezea
uhusiano wake ndani ya Mungu mmoja wa kweli na anawataka mitume na wafuasi
watambue na wakubali kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, na kwamba Mungu ni Baba
yake, na kwamba Roho Mtakatifu alitumwa kwao na Baba na Mwana. Wakristo wa
kwanza walisadiki ndani ya Utatu Mtakatifu bila kupinga. Baada ya kuamini,
kinachofuata ni Upendo. “Kama mtu akinipenda mimi” Yesu anasema, “Baba yangu
atampenda. Nasi tutakuja kwake nakufanya makao ndani yake.”
“…(Wana ndoa) matunda ya
wana ndoa yanakuwa ishara ya kuelewa na kuelezea fumbo la Mungu mwenyewe,
kwasababu kwa mtazamo wa Kikristo wa Utatu mtakatifu, Mungu anatafakariwa kama
Baba, na Mwana na Roho Upendo. Utatu Mtakatifu ni umoja wa upendo, na familia
ndiyo inayoishi kuonesha umoja huu. Mtakatifu Papa Yohane Paulo wa Pili, alitoa
mwanga kwa hili alivyosema ‘Mungu wetu katika undani wake sio upweke bali ni
familia, kwani ndani yake ana Ubaba, mwana na undani wa familia ambaye ni
Upendo. upendo huo ndani ya familia ya Kimungu ni Roho Mtakatifu’”. (Baba
Mtakatifu Fransisko katika Furaha ya upendo, Amoris Laetitia, 11)
Tutafakari leo juu ya
sherehe hii ya Utatu Mtakatifu, ni mara ngapi nina enzi upendo huu wa Utatu
Mtakatifu katika mahusiano yangu? Tujaribu kufanya jitihada tusonge mbele
zaidi, katika mapendo yetu, na kumruhusu Mungu akupe matokeo mazuri ya tokanayo
na upendo wako kwake na kwa jirani.
Sala: Baba na Mwana na
Roho Mtakatifu, nisaidie mimi niweze kuku fahamu wewe na kukupenda. Nisaidie
niweze kuelewa upendo unaoshiriki na Mwanao. Kwa kuelewa upendo huo, nisaidie
na mimi niweze kushirikisha upendo huo kwa wengine. Baba na Mwana na Roho
Mtakatifu, nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment