MASOMO YA MISA,
JUNI 26, 2022
DOMINIKA YA 13
YA MWAKA C
SOMO 1
1 Fal. 19:16b.
19-21
Bwana alimwambia
Eliya: Enenda, mtie mafuta Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola awe nabii
mahali pako. Basi akaondoka huko, akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa
akilima, mwenye jozi za ng’ombe kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe
alikuwa pamoja na lile la kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa
vazi lake juu yake. Naye akawaacha ng’ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe
ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata.
Akamwambia, Enenda, urudi; ni nini niliyokutendea. Akarudi akiacha kumfuata,
akatwaa lile jozi la ng’ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya
ng’ombe, akawapa watu, wakala. Kisha akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA
KATIKATI
Zab16:1-2, 5,
7-11 (K) 5
(K) Bwana ndiye
fungu la posho langu.
Mungu,
unihifadhi mimi,
Kwa maana
nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia
Bwana, Ndiwe Bwana wangu;
Bwana ndiye
fungu la posho langu.
Na la kikombe
changu;
Wewe unaishika
kura yangu. (K)
Nitamhimidi
Bwana aliyenipa shauri,
Naam, mtima
wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka Bwana
mbele yangu daima,
Kwa kuwa yako
kuumeni kwangu, sitaondoshwa. (K)
Kwa hiyo moyo
wangu unafurahi,
Na utukufu wangu
unashangilia,
Naam, mwili
wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Maana
hutakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa
mtakatifu wako aone uharibifu. (K)
Utanijulisha
njia ya uzima;
Mbele za uso
wako ziko furaha tele
Na katika mkono
wako wa kuume
Mna mema ya
milele. (K)
SOMO 2
Gal. 5 :1,13-18
Katika ungwana
huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simamemi, wala msinaswe tena chini ya
kongwa la utumwa. Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu
usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote
imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi
yako. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana. Basi nasema,
Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili
hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi
zimepingama, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo
chini ya sheria.
Neno la Bwana...
Tumshukuru Mungu
SHANGILIO
Yn. 17:17
Aleluya,
aleluya,
Neno lako ndiyo
kweli, ee Bwana; Ututakase sisi kwa ile kweli.
Aleluya.
INJILI
Lk. 9:51-62
Ikawa, siku za
kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, Yesu aliukaza uso wake kwenda
Yerusalemu; akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia
katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. Lakini wenyeji
hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. Wanafunzi
wake Yakobo na Yohane walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto
ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? Akawageukia
akawakanya. Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo. Kwa maana Mwana
wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda
mpaka kijiji kingine. Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia,
Nitakufuata ko kote utakakokwenda. Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege
wa angani wana vioto, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.
Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende kumzika
baba yangu. Akamwambia, Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda
ukautangaze ufalme wa Mungu. Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana nitakufuata;
lakini, nipe ruhusu kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia,
Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa
Mungu.
Neno la Bwana...
Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright ©
2022, "MASOMO YA MISA" published by T.M.P. Book Department, Tabora –
Tanzania. Readings reproduced by Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment