“ASALI
ITOKAYO MWAMBANI”
Jumamosi,
Juni, 21, 2025,
Juma
la 11 la Mwaka wa Kanisa
2 Kor 12:1-10
Zab
88: 4-5, 29-34;
Mt 6:
24-34
BWANA
WANGU NINANI- MUNGU AU PESA?
“Moyo
uliogawanyika ni moyo wa huzuni.” Wote
tunajua hili kwasababu ni moyo ulio na wasi wasi na usiojiweza. Leo tunasikia
Yesu akituambia hatuwezi kutumikia mabwana wawili. Hatuwezi kujitoa kwa Mungu
moja kwa moja kama tumetekwa na pesa. Kwanini? Kwasababu vyote vinahitaji
kujikita na kujitoa. Mungu anahitaji majitoleo ya kweli si kwaajili yake bali
kwaajili yetu wenyewe. Hatuwezi kuwa na furaha kabisa au furaha ya kweli bila
Mungu. Na ni Mungu mwenyewe anaweza kurudhisha tamaa ya moyo wa Mwanadamu.
Hakuna
mtu anaeweza kuwatumikia mabwana wawili kwa muda mrefu. Kwasababu wakati
Mabwana wote wawili wakiwa wanatembea pamoja, anaweza kuwafuata nyuma yao
lakini watakapo amua mmoja kwenda uelekeo wake na huyu wake, lazima achague ni
yupi wakumfuata. Haijalishi ni mara ngapi watu wamemuasi Mungu na kufuata au
kuabudu mali na pesa, Mungu haachi kamwe kuwapigania warudi kwake. Tujikumbushe
maneno haya ya Mungu “Sitawaacha kamwe wala kuwakataa ninyi” (Kumb 31: 6). Somo
la kweli katika historia ya Mwanadamu ni kwamba-Hakuna mtu anayeweza
kuwatumikia mabwana wawili katika hali ya kweli. Mkristo kwa kweli hawezi
kutenda haki ya Mungu kwakujiingiza kabisa katika mali na anasa za ulimwengu
huu.
Uovu
wa kujaribu kugawanya uaminifu wetu unajikita katika kushindwa kwetu kutumainia
Upendo wa Mungu Baba yetu. Tunajaribu kutafuta ulinzi wa maisha yetu katika
mali na utajiri wetu. Tunafanya kila liwezekanalo kulinda heshima yetu katika
mali, tunadhani tukipungukiwa tutadharauliwa na watu, kwahiyo siku zote
tunajaribu kujilinda kuweka mambo yetu vizuri bila kujali kama na muumiza
mwanadamu mwenzangu. Tunawatumikisha wengine wanateseka bila maji au chakula,
ali mradi nimepata faida na utajiri wangu ubaki pale pale. Tunaogopa kuwasaidia
wengine kwasababu tunadhani tutapungukiwa. Roho na akili yetu haina Amani usiku
kucha kwasababu natafuta jinsi ya kutegemeza utajiri wangu, tumekamatwa sana na
mali mpaka tunasahau nafsi ya Mungu katika maisha yetu. Tunakimbilia kwenye
biashara kiasi chakushindwa hata kufanya ishara ya msalaba ili Mungu abariki
mipango yetu. Mungu ni namba moja, mengine yote ni sifuri, tujitahidi
kuitanguliza hii numba moja ili hizi sifuri zinazofuata nyuma yake zifanye yote
yawe mengi, lakini ukitanguliza sifuri badala ya moja nadhani unajua utapata
nini.
Kwa
ufupi maisha yetu yatawaliwe na Mungu, chochote kamwe kisichukue nafasi ya
Mungu. Mungu anapenda maadili yetu na thamani ya yote tulionayo yajengwe katika
msingi wake yeye mwenyewe na hapo yataleta furaha na Amani kwetu. Mungu anajua
mahitaji yetu hata kabla hatuja mwomba na anawapa wote kwa upendo wanao
mtumainia.
Sala:
Bwana naomba usinifanye maskini wala usinifanye tajiri mno, nishibishe kwa
chakula ninacho hitaji nisije nikashiba mno nikakutukana nikasema “Mungu ni
nani kwani?” au nisiwe maskini mno nikaiba nikalikashifu jina lako Mungu.
Amina. (Hii ni sala ya kiasi) (Prayer of balance).
Thanks
ReplyDelete