“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumatano, Aprili 24, 2024.
Juma la 4 la Pasaka
Mdo 12:24-13:5;
Zab 67:2-3,5-6,8 (K. 4);
Yn 12:44-50.
YESU, MWANGA KWA
ULIMWENGU!
Kumfahamu Yesu ni
kumfahamu Baba pia. Ukweli ni kwamba uwepo wa Baba umefunikwa kama Umungu wa
Kristo ulivyo funikwa. Ingawaje hatuna uzoefu wa kumuona Yesu akitembea kama
wale wafuasi wa kwanza walivyo muona, tunakutana na ukweli huo huo katika
Ekaristi Takatifu. Wakati tunapo ingia kanisani na kupiga goti kuelekea
Tabernakulo, ni vizuri kuwa na uelewa na kufahamu kuwa tupo mbele ya uwepo wa
Mungu Mwana. Na kwa njia hiyo tupo pia mbele ya uwepo wa Mungu Baba! Uwepo wao
ni wazi na hakika. Ni kwasabau tu wamefichwa kutoka katika milango yetu mitano
ya fahamu.
Katika Injili, Yesu
anakuja kama nuru ili tusiwe tena kwenye giza. Anakuja kwa lengo hili:
tumuamini yeye na kuwa na ukweli na uzima. Zaburi ya 27 mstari wa 1, unasema
“Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu”. Kama ilivyo mwanga wa kawaida hufunua
kile kilicho fichwa kwanye giza, vivyo hivyo Neno la Mungu huleta nuru ili
tuweze kutambuaa ukweli ulio fichika ndani ya Ufalme wa Mungu. Kama nuru,
huleta furaha na uzima kwa wengine. Inafanya mbegu ya imani ikue ndani yetu,
ili tuweze kushiriki furaha ya Mungu na uzima na wengine. Sisi mara nyingi
tunachagua kubaki kaburini kama Mafarisayo bila kufufuka. Lakini Yesu ni mlango
wa uzima wa milele. Kwani Yesu ni uzima na ufufuo na wote wale wanao mwamini
watakuwa na uzima wa milele.
Sala: Bwana, nisaidie
niweze kukuelewa wewe na kukupenda wewe na katika uhusiano huo niweze kumfahamu
na kumpenda Baba na Roho Mtakatifu. Bwana, ninaomba wewe uwe mwanga ambapo kwa
njia yako niweze kukuona wewe na ulimwengu. Yesu nakuamini wewe. Amina.
No comments:
Post a Comment