MASOMO YA MISA, MEI 10, 2023
JUMATANO, JUMA LA 5 LA PASAKA
SOMO 1
Mdo. 15:1-6
Siku zile, walishuka watu waliotoka Uyahudi
wakawafundisha wale ndugu ya kwamba, Msipotahiriwa kama desturi ya Musa hamwezi
kuokoka. Basi baada ya Paulo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhojiana
nao Sana, ndugu wakaamuru kwamba Paulo na Barnaba na wengine miongoni mwao
wapande kwenda Yerusalemu kwa mitume na wazee kwa habari ya swali hilo.
Basi, wakisafirishwa na kanisa, wakapita kati ya
nchi ya Foinike na Samaria, wakitangaza habari za kuongoka kwao Mataifa;
wakawafurahisha ndugu sana. Walipofika Yerusalemu wakakaribishwa na kanisa na
mitume na wazee, nao wakawaeleza mambo yote Mungu aliyoyafanya pamoja nao.
Lakini baadhi. ya madhehebu ya Mafarisayo
walioamini wakasimama wakisema, Ni lazima kuwatahiri na kuwaagiza kuishika
Torati ya Musa. Mitume na wazee wakakusanyika wapate kulifikiri neno hilo.
Neno la Bwana... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 122:1-5 (K) 1
(K) Nalifurahi waliponiambia, Na Twende nyumbani
kwa Bwana.
Nalifurahi waliponiambia
Na twende nyumbani kwa Bwana.
Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, ee Yerusalemu. (K)
Ee Yerusalemu uliyejengwa
Kama mji ulioshikamana,
Huko ndiko walikopanda kabila,
Kabila za Bwana. (K)
Ushuhuda kwa Israeli,
Walishukuru jina la Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. (K)
SHANGILIO
Yn. 10 :14
Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi mchungaji mwema, nao walio wangu
nawajua, nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.
INJILI
Yn. 15 :1-8
Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mimi
ndimi mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu
lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa. Ninyi
mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya lile neno nililowaambia. Kaeni ndani yangu,
nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisi- pokaa ndani
ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani
yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya
neno lo lote. Mtu asipokaa ndani yangu, hutupwa nje kama tawi na kunyauka; watu
huyakusanya na kuyatupa notoni yakateketea.
Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu
yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa. Hivyo hutukuzwa Baba
yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu.
Neno la Bwana... Sifa kwako Ee Kristo
Copyright © 2023, "MASOMO YA MISA"
published by T.M.P. Book Department, Tabora – Tanzania. Readings reproduced by
Furaha ya Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment