“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Jumatano, Mei 10, 2023
Juma la 5 la Pasaka
Mdo 15:1-6;
Zab 122:1-5 (R. 1);
Yn 15:1-8.
KUONDOA MAJIVUNO NA UBINAFSI!
Kupunguza matawi ni muhimu kwa mti kama unapenda uzae
mataunda mazuri au maua mazuri. Kama, kwa mfano, mti wa maua ya waridi unakuwa
bila kupunguzwa, unatoa vimaua vidogo vingi, amabavyo ni dhaifu. Lakini kwa mti
mzuri ulio pruniwa unatoa maua mazuri yenye afya. Yesu anatumia mfano kama huu
kutufundisha somo kama hilo katika kuzaa matunda mazuri kwa ufalme wake.
Anataka maisha yetu yawe yenye matunda mema na anataka kututumia sisi kama
vyombo vyake vyenye nguvu ulimwenguni. Lakini tusipo ingia katika maisha ya
kiroho ya kujipruni mara kwa mara , hatutakuwa vyombo ambavyo Mungu anaweza
kuvitumia.
Kujipruni kiroho unachukua ile hali ya kumruhusu Mungu
aondoe maovu katika maisha yetu ili fadhila ziweze kungaa. Na hili lina
fanikiwa hasa tunapo mruhusu atupe unyenyekevu na kutuondoa katika maringo
yetu. Hili linaweza kuumiza, lakini maumivu yanayo tokana na kunyenyekeshwa na
Mungu ni ufunguo wa kukuwa kiroho. Kwa kukuwa katika unyenyekevu, tunakuwa
zaidi katika kujikita katika chanzo chetu kuliko katika kukuwa katika hali zetu
wenyewe, mawazo yetu wenyewe na mipango yetu wenyewe. Mungu katika hali ya juu
kabisa ana hekima kuliko sisi na kama tutaendelea kumwelekea kila mara kama
chanzo chetu, tutakuwa wenye nguvu zaidi na kujiandaa yeye afanye mambo makubwa
zaidi kwa njia yetu.
Kujiruhusu kupruniwa kiroho maana yake ni kuachia
yaondoke mapenzi yetu wenyewe na mawazo yetu. Maana yake tunaachia kujitawala
wenyewe na kumwachia aliye mkuu wa kukuza akuze na kuchukua nafasi. Ina maana
tuna mwamini yeye zaidi kuliko tunavyo jiamini sisi wenyewe. Hili linahitaji
kufa kwa nafsi zetu wenyewe na unyenyekevu wa kweli na kukiri kabisa kwamba
Mungu ndiye tegemeo letu kwa kila kitu, kama tawi linavyo tegemea mti. Bila
mti, tutaseka na kufa. Mwamini yeye na mipango yake na tambua kuwa hii ndio
njia pekee ya kuzaa matunda mema, ambayo Mungu anayataka kupitia wewe.
Sala: Bwana, ninakuomba upruni majivuno yangu na kuyatupa
mbali na pia uovu wangu. Nitakase mimi kutoka katika dhambi zangu nyingi ili
niweze kujikabidhi kwako kwa kila kitu. Na ninapo jifunza kujikabidhi kwako,
ninakuomba uanza kuzaa matunda mema katika maisha yangu. Yesu, nakuamini wewe.
Amina.
Copyright ©2013-2023 ©FurKat, Furaha ya
Kikatoliki: see www.fur-kat.blogspot.com
No comments:
Post a Comment