
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Jumanne, Aprili 8, 2025,
Juma la 5 la Kwaresima
Hes 21: 4-9;
Zab 101: 2-3, 16-21;
Yn 8: 21-30.
UHUSIANO WETU NA MUNGU
Katika somo la kwanza tunasikia waisraeli wakimlalamikia Mungu na
Musa. Hawa watu walikombolewa kutoka utumwani, lakini wanataka tu kurudi tena
huko utumwani. Hawaku mfahamu Mungu, aliye wakomboa. Hawakuwa na uhusiano wa
kweli naye. Katika somo la Injili tunamuona Yesu anavyo jali, na upendo wake
kwa wanadamu. Karne baada ya karne waliwasikia manabii, na walitegemea Masiha.
Lakini aliposimama kati yao walishindwa kumtambua. Uelewa wao kuhusu Masiha
haukuwa kamili. Yesu anajaribu kuwaamsha kwa mafundisho yake.
Baba ndiye aliye mtuma Yesu ulimwenguni kwa utume na Yesu anakiri
kwamba Mungu hawezi kumwacha. Yesu anatambua hili na anafurahia Baraka za
Kimungu kwa muunganiko huu. Tofauti na Waisraeli na mafarisayo, Yesu anatambua
uhusiano wake na Baba.
Sisi tunaweza kuwa “Wakristo walio lala”. Tunafahamu kusali,
tunafahamu ni muda ghani wa kusimama, wakati wa kupiga magoti, wakati wa kukaa
tukiwa kanisani, lakini uhusiano wetu na Mungu ni wakati tu tukiwa na furaha.
Tunaanza kuwa na wasi wasi na Mungu tunapo kumbani na Matatizo. Liturjia ya leo
inatutaka tuwe wakristo tulio amka, kuwa na uelewa na uhsiano wetu na Mungu na
pia kuelewa mambo ya ulimwengu. Yesu kwa sadaka yake msalabani ametukomboa
kutoka katika utumwa wetu wa dhambi. Kipindi hichi cha kwaresima tunaitwa kuwa
wapya katika mapendo na Mungu, kumgeukia Yesu msalabani na kutafuta upendo,
msamaha na huruma kutoka kwake, na kuwa upendo na huruma kwa wengine.
Tafakari leo juu ya utume aliopewa Yesu: maisha yake ya kujitoa
sadaka. Tafakari jinsi Mungu anavyopenda tuishi utume huu kwa maisha ya sadaka
ya upendo na kujitoa. Unaweza kuwa uyaishi kwa moyo wako wote, au unaweza kuwa
unahitaji kuelekezwa upya. Sema “ndio” kwa mapenzi yake kwa ujasiri na ushujaa
na Mungu atatembea nawe katika kila hatua ya maisha yako.
Sala: Bwana, ninasema “ndio” kwa mpango kamili ulionao katika
maisha yangu. Vyovyote itakavyokuwa ninakubali bila kuwa na mashaka, Bwana
mpendwa. Ninatambua upo na mimi daima na sipo mwenyewe. Yesu nakuamini wewe.
Amina
No comments:
Post a Comment