
“KUFUFUKA NA KRISTO”
Tafakari ya Pasaka
Alhamisi, Aprili 24, 2025.
Oktava ya Pasaka
Mdo 3:11-26
Zab 8:2,5-9
Lk 24:35-48
UFUFUKO: KUONDOA HOFU NA KUKUMBATIA FURAHA!
Wakati Wanafunzi wawili wakiwa wanashirikisha
habari juu ya tukio la Emaus, Yesu alitokea kati yao, walishtuka na kuogopa.
Yesu katika hali yake ya Kibinadamu yakuonesha makovu ya madonda yake, kwa kula
chakula pamoja nao, iliwafanya waondoe hofu na kuondoa baadhi ya maswali
yaliokuwa yakiwasumbua. Walimuona Yesu, Bwana wao mpendwa, ambaye amejifunua
mwenyewe, ambaye ni muelewa, ambaye anawasiliana nao, ambaye anasamehe na
ambaye anawapa nguvu. Waliyapokea maneno yake katika hali ya juu sana, na
wanafanywa kuelewa habari yote kuhusu maisha ya Yesu. Watu ambao walifikiri
kwamba maisha yao yamefika mwisho na ulimwengu wao umekwisha, walianza kuona
mwanzo wa Ulimwengu mpya.
Hali hii ya Wafuasi inafunua hali ambayo hata
sisi tunakutana nayo wakati Mungu anatuita tuingie katika utukufu na neema
yake. Mara nyingi wakati Mungu anavyotuita karibu naye, wakati anatuita tuweze
kuona furaha ua ufufuko, tunapatwa na mashaka. Tunaweza tukaona ngumu kupokea
ukweli wa ufufuko katika maisha yetu. Hii inaweza kutokea kwasababu mbali
mbali. Kukata tamaa inaweza kuwa sababu yetu kushindwa kukumbatia maisha ya
ufufuko. Wafuasi walikatishwa tamaa kabisa kwa kifo cha Kristo. Na sasa kwamba
amefufuka, na alikuwa amesimama mbele yao, walikuwa na wasi wasi kuachia hali
hiyo ya kukata tamaa iondoke.
Sisi pia, tunaweza tukaacha uzito wa
ulimwengu, dhambi zetu au dhambi za wengine, zitukatishe tamaa. Tunaweza
kusikia hasira na kuchukia na tukajikuta tunashindwa kutoka katika matatizo
tunayo kutana nayo. Kuwa na furaha ya ufufuko maana yake tunarudisha macho yetu
na kuangalia ule ukweli ambao Mungu anapenda sisi tuutazame. Haina maana ya
kukatishwa tamaa kwa matatizo mbali mbali yanayo kuja katika njia zetu. Au
kushindwa kumfuata Mungu kwasababu ya dhambi za wengine. Mungu wetu anatuita
tutazame kitu kingine kikubwa zaidi kuliko matatizo yetu. Anatuita kwenye
ushindi wake. Kutazama katika ushindi wake ni kuwa huru na kuwa na Imani ya
hali ya juu katika maisha yetu. Na Imani hiyo kwa Bwana mfufuka itakuwa na
furaha ya ajabu ambayo Mungu anataka tuwe nayo. Kwa macho yake yakiwa yame
elekezwa kwake, yote yale yanayo kushawishi ukate tamaa yataondoka.
Sala: Bwana, ninataka kukutazama wewe.
Ninataka kukuona wewe ukiwa umefufuka katika wafu na nichukue furaha kubwa
katika ukweli huu. Nisaidie, niweze kuhisi furaha kuu inayotoka kwa kukujua
wewe, Bwana wetu mfufuka. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment