
“KWARESIMA YA UKARIMU”
Tafakari ya Kwaresima
Ijumaa, Aprili, 4, 2025,
Juma la 4 la Kwaresima
Hek 2: 1, 12-22;
Zab 34: 17-21, 23;
Yn 7: 1-2, 10, 25-30.
KUWEKA MAJARIBUNI
Kitabu cha Hekima kina kadiriwa kuandikwa
miaka mia kabla ya kuja Kristo. Lakini cha kushangaza maelezo yake yanaonekana
kuwa karibu sana katika kumwelezea Yesu. Somo la leo linaongelea kuhusu mtu
ambaye anamjua Mungu na hata anajiita “Mtumishi wa Mungu” (Hek 2:3). Na kama
Yesu, huyu mtu ana adui ambao wanamfuatilia ili kumtega katika maneno yake na
hata kutaka kumua. (2:19-20).
Leo tunakumbushwa kwamba kutakuwa na upinzani
daima juu ya Kristo na wale wanao mfuata. Katika somo la Injili, tunasoma, juu
ya kushindwa kwa jaribio la kumkamata Yesu wakati wa sikukuu ya Tabernaklo
kwasababu “saa yake bado” (Yn 7:30). Ni kweli, Yesu alisulubiwa na kufa, lakini
kifo hakikuweza kumweka chini. Mungu alimfufua! Ndivyo hivyo sisi Mungu
hataruhusu kitu tunacho vumilia kituangushe bila kutusaidia. Atatuimarisha.
Atatupa neema. Atatuinua tena.
Yesu anatuita sisi tuwe mabalozi wake.
Anatutaka sisi tushirikishe habari njema kwa kila mtu tunae kutana naye. Huu
ndio wito wa pekee, lakini pia kuna changamoto zake. Pengine juhudi zetu
zitafanikiwa baada ya kupata upinzani mkubwa na majaribu makubwa, na hata
changamoto nyingine ni za kusukumwa. Lakini tukibaki imara katika kushirikisha
Injili kwa upendo na sio kwa kujiona wema wenyewe, kwa furaha na sio hasira,
tutabarikiwa sana. Yesu atatuambia “vyema mtumwa mwema ingia katika furaha ya
Bwana wako” (Mt 25:21). Hauhitaji kuwa mtu uliye bobea katika kuongea au kuwa
mashuhuri katika kuongea. Wala haupaswi kuwa na nguvu labda nyingine. Tunapaswa
kutambua tu Yesu anatupa nguvu na neema tunapo amua kumshuhudia. Na neema yake
itatutunza kama ilivyo na nguvu ya kuwavuta watu kwake.
Sala: Bwana, nakupenda. Nisaidie nikuone na
kukupenda wewe katika jirani zangu. Nisaidie ninapo wekwa katika majaribu, na
familia yangu, marafiki zangu, na wengine wanao nipinga kwasababu ya
kukutangaza wewe na thamani ya Injili yako. Tufariji daima tunapo tangaza
Injili yako. Tupe nguvu yako ya Kimungu. Yesu nakuamini wewe. Amina
No comments:
Post a Comment